Na Mwandishi Wetu, Morogoro

SERIKALI mkoani Morogoro imewahimiza Wafanyabiashara wakubwa eneo hilo kukitumia Kituo cha Biashara kilichofunguliwa na Benki ya NMB ili kutambua fursa zilizopo katika kituo hicho pamoja na kuunganishwa na masoko ya ndani na nje hatua itakayo saidia kukuza uchumi wa mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Steven Kebwe alisema hayo wakati akizindua kituo hicho cha kibiashara mkoani Morogoro kilichoanzishwa na Benki ya NMB kwa lengo la kuwasaidia wafanyabiashara wa mkoa huo.

Katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo, alisema NMB imeamua kuanzisha kituo hicho cha kibiashara baada ya Mkoa wa Morogoro kuwa na fursa nyingi za kiuchumi ikiwemo shughuli za kilimo, uchimbaji madini na masuala ya kiutalii.

Alisema kuwa NMB kupitia fursa hizo imeona iwasaidia Wafanyabiashara wa Morogoro kwa kuanzishia kituo maalumu ambacho licha ya kupata elimu na kuunganishwa na masoko ya ndani na nje pia watapatiwa huduma anuai za mikopo.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker alisema kituo cha Biashara cha Morogoro ni kituo cha kumi nchini na kimeanzishwa mahususi kwa ajili ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Morogoro waweze kukuza uchumi wao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akizungumza 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...