Na Mwandishi wetu
IMEELEZWA kuwa katika mazingira ya sasa ya kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati kwa kuwa na viwanda ni lazima taifa litakuwa na mabadiliko katika makazi na kwamba miji mingi itachipuka.
Aidha serikali inapotekeleza mpango wake wa pili wa maendeleo 2016/17-2020/21 katika mpango wa muda mrefu wa maendeleo kwa lengo la kuwezesha mabadiliko ya kiuchumi kwa maendeleo ya watu uwepo wa miji ni wa lazima.
Aidha mazingira duni ya maisha katika vijiji kunafanya watu kuhamia katika maeneo yenye shughuli mbalimbali na hivyo kukuza miji iliyopo.
Hayo yalisemwa na Dk Lorah Basolile Madete, Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha kwenye mkutano wa mkutano wa 5 wa jukwaa la ukuaji wa miji Tanzania (Tanzania Urbanisation Laboratory - TULab) ulioambatana na uwasilishaji wa tafiti tatu zilizofanywa na TUlab kuanzia mwaka jana.
Pia alisema tofauti kubwa ya kipato iliyopo vijijini na mijini inafanya maeneo ya jirani na vijiji kubadilika na kuanza kuchukua muonekano wa miji.
“Ndio kusema ni lazima kujiandaa kwa mabadiliko hayo na kuwa na mpangilio wa kudhibiti ukuaji wa miji, kinyume chake Tanzania haitaweza kuvuna faida katika uchumi, kijamii na kimazingira kama miji itakua ghafla bila mipango mathubuti” alisema Dk Madete.
Katika mkutano huo ilielezwa kuwa kudhibiti miji ni kitu muhimu ikiwa mataifa yanataka kuwa na maendeleo endelevu ya kiuchumi na ustawi wa jamii.
Miji hiyo inatakiwa kupangwa na kukua kwa mujibu wa makubaliano ya dunia kama yale ya Paris na maendeleo endelevu yaliyokubaliwa na Umoja wa Mataifa.
Mkuu
wa Utawala na Rasilimali Watu wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na
Kijamii (ESRF), Bw. Deodatus Sagamiko akitoa neno la ukaribisho kwa
niaba ya Mkurugenzi wa ESRF Dk Tausi Kida wakati wa Mkutano wa 5 wa
maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika
ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Mchumi
Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Lorah Basolile Madete
akitoa neno la ufunguzi wakati wa Mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa
miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa
Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
Bw.
Anton Cartwright wa Kituo cha Afrika cha miji kutoka nchini Afrika
Kusini akiwasilisha Muhtasari wa tafiti tatu zilizofanyika chini ya
Maabara inayoshughulikia mabadiliko kuelekea miji Tanzania (TULab) na
kuongoza majadiliano kuhusu athari za kisera katika tathmini ya kitaifa
ya mabadiliko kuelekea miji (National Urbanization Transition Assessment
-NUTA) wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania
uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya
Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
Mratibu
wa Maabara inayoshughulikia mabadiliko kuelekea miji Tanzania (TULab)
kutoka ESRF, Reshian W. Kanyatila akielezea masharti ya ushiriki katika
shindano la utoaji huduma katika majiji.
Mtafiti
Msaidizi na Mratibu wa Miradi wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Bw. Emmanuel
Njavike (katikati) akiwasilisha waliyojadili katika kikundi kazi wakati
wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya washiriki wakitoa maoni wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji
wa miji Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya
Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jana jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...