Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
UVUVI na uuzaji wa samaki katika soko la Feri jijini Dar es salaam umezidi kuimarika katika mchakato mzima wa uvuvi wa samaki wenye viwango vinavyotakiwa na uuzwaji wake sokoni umekuwa na tija.

Akizungumza na blogu ya jamii Kaimu Afisa Uvuvi wa soko la Feri Ahmed Mbarouk ameeleza kuwa upatikanaji wa samaki kwa sasa ni mzuri hasa kwa samaki wakubwa  na hata mauzo yamekuwa mazuri pia kutokana na ubora wa samaki wanaovuliwa kuwa na viwango.

Kuhusiana na kutokomeza uvuvi haramu Abdallah ameeleza kuwa kwa sasa hakuna matukio hayo ya wavuvi kutumia baruti kuvua samaki na hii ni baada ya kampeni waliyoiendesha na kufanikisha kukamatwa kwa nyavu haramu kubwa 14 aina ya kokoro ambazo ziliteketezwa.

Akieleza changamoto wanazokabiliana nazo kiutendaji Afisa uvuvi huyo amesema kuwa vifaa vya kazi hasa boti la doria limekosekana hali inayowapelekea kufanya doria kwa miguu licha ya kuwa na askari wa Suma JKT wanaosaidia na kueleza kuwa boti hilo likipatikana litawarahisishia kazi ya kufanya doria nyakati zote na kwa uhuru zaidi.

Aidha ametoa wito kwa  kwa wavuvi kwa kuvua samaki wenye viwango vinavyofaa na doria hizo ni endelevu hivyo wavuvi wafuate kanuni na taratibu.

Mmoja wa wavuvi hao Jumanne Ramadhani amesema kuwa wanaushukuru uongozi wa soko hilo hasa maafisa uvuvi kwa kuwapa elimu na kuwasimamia kwani hadi sasa wanajua viwango vya samaki wanaotakiwa kuvuliwa na kupelekwa sokoni na kwa sasa biashara ni nzuri kwani upatikaji wa samaki hasa wakubwa umekuwa mkubwa na soko kwa ujumla limesimama imara.
 . Afisa uvuvi  Msaidizi katika soko la samaki Feri Ahmed Mbarouk akizungumza na blogu ya jamii kuhusiana na hali ya uvuvi na biashara ya samaki sokoni hapo.
 Samaki wakiwa tayari kwa mauzo ambapo samaki mmoja huuzwa kati ya shilingi 45,000 hadi 50,000.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
 Mnada wa samaki ukiendelea katika soko la samaki la Feri jijini Dar es Salaam.
Mwandishi kutoka Michuzi blog akiangalia samaki aina ya kaa mara baada ya kuvuliwa na mmoja wa wavuvi.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...