Na Mwandishi Wetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) amewaagiza wajumbe wa baraza la chama cha walimu Tanzania kutekeleza hoja zilizotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Hayo ameyasema hii leo wakati wa kikao cha dhararu kilichowakutanisha wajumbe hao kujadili hoja zote zilizotolewa na mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) katika taarifa yake ya mwaka 2016/2017.

Waziri Mhagama alieleza kuwa ripoti ya mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) imeelezea changamoto zilizokuwepo kwenye chama hapo awali ikiwemo masuala ya mapato na matumizi ya chama, mfumo wa uongozi na uwajibikaji, mikataba iliyoingiwa na chama ya uwekezaji, suala la utozaji ada kwa wananchana na mfumo wa sera ya malipo ya fedha.

“Wajumbe wa baraza hili mkishiriki kikamilifu katika kujadili na kufikia maamuzi ya pamoja ili kutimiza malengo ya chama na kutakuwa na utaratibu utakao saidia kuongeza uwazi na mshikamano miongoni mwa wanachama” alisisitiza Mhagama.

Aliongeza pia kwa kuyatekeleza hayo chama kitakuwa na utaratibu mzuri utakao heshimiwa na kila kiongozi wa chama na wanachama wote pamoja na namna bora ya kutunza na kutumia fedha za chama ili ziweze kutumika katika utoaji wa huduma mbalimbali kwa manufaa ya wanachama wote.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza wakati wa mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) leo Jijini Dodoma. Baraza hilo limekutana ili kujadili masuala yanayohusu chama hicho ikiwa ni pamoja na ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipongezwa na Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bi. Leah Ulaya (katikati) mara baada ya kumaliza hotuba yake wakati wa mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la chama hicho leo Jijini Dodoma. Baraza hilo limekutana ili kujadili masuala yanayohusu chama hicho ikiwa ni pamoja na ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Kushoto ni Katibu Mkuu wa CWT, Bw. Deus Seif.
 Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoke akizungumza wakati wa mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) leo Jijini Dodoma. Baraza hilo limekutana kujadili masuala yanayohusu chama hicho ikiwa ni pamoja na ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG). (Wapili kutoka kulia) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akifurahia jambo na Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bibi. Leah Ulaya (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Walimu Wenye Ulemavu (CWT) Taifa, Mwl. Ulumbi Shani (katikati) mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la chama hicho leo Jijini Dodoma. Baraza hilo limekutana ili kujadili masuala yanayohusu chama hicho ikiwa ni pamoja na ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kutoka mikoa ya Rukwa na Ruvuma mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la chama hicho uliofanyika hii leo Jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...