WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba apeleke wataalamu kwenye kituo cha utafiti kilichopo Makutupora, Dodoma ili wazalishe mbegu bora za ufuta kwa ajili ya mikoa ya kanda ya kati.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Septemba 20, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mauno, wilayani Kondoa ambako alienda kukagua ujenzi wa kituo cha afya. Waziri Mkuu leo ameanza ziara ya kikazi ya siku saba katika mkoa wa Dodoma.

Alikuwa akijibu ombi la mbunge wa viti maalum, Bi. Mariam Ditopile ambaye alisema mkoa wa Dodoma ni wa pili kwa uzalishaji wa ufuta hapa nchini lakini aina ya ufuta inayozalishwa ni ya daraja la chini kwa sababu hawana mbegu za ufuta mweupe.

“Ili mradi mikoa ya kanda ya kati inazalisha ufuta, ninamuagiza Waziri wa Kilimo ahamishe watumishi kutoka kokote ili wakae Makutupora na kuwasaidia wakulima wawe na mbegu bora zenye kutoa mafuta mengi,” alisema.

Amesema kila mwaka Serikali inatumia zaidi ya dola za Marekani milioni 267 kuagiza mafuta ya kula kutoa nje ya nchi na kwamba hivi sasa imeamua kufufua mazao ya mbegu za mafuta ili mafuta ya kula yazalishwe kwa wingi hapa nchini.

 “Sasa hivi tumeanza kufufua mazao ya mbegu za mafuta ni nilianza mkoa wa Kigoma kwa kuhimiza kilimo cha michikichi. Sasa hivi niko Dodoma nahimiza ufuta na alizeti na nitaenda Singida kwa ajili ya zao hilo la alizeti,” amesema.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza wananchi wa Kata ya Mauno wilayani Kondoa, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018.  
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, akizungumza na wananchi wa Kata ya Mauno Kondoa Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018.

 Wananchi wa Kata ya Mauno wilayani Kondoa, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipowasili katika kata hiyo akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia chumba cha kuhifadhia maiti, wakati alipokagua ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya Mauno Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018, kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Godwin Mkanwa, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dk. Ikaji Rashid.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...