WAZIRI MKUUKassim Majaliwa amesemalishe duni pamoja na ulaji usiofaa na mitindo ya maisha vinachangia kwa kiasi kikubwa katika ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza hususan kwa vijana na watu wazima, ambao ndiyo nguvu kazi kwa Taifa. 
“Ni jambo lisilopingika kuwa hatua za kukabiliana na magonjwa ya kusendeka (mfano matatizo ya moyo, saratani, kisukari na shinikizo kubwa la damu) zinachangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza kasi ya maendeleo yetu kwani gharama za matibabu yake ni kubwa mno; si kwa kaya zinazoathirika tu bali kwa Taifa zima.” 
Waziri Mkuu  ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Septemba 11, 2018),  wakati akifungua mkutano wa tano wa wadau wa masuala ya lishe, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kambarage, Hazina jijini Dodoma.  
Waziri Mkuu amesema lishe iliyozidi inadhihirishwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukizwa yanayotokana na mabadiliko ya mitindo ya maisha na ulaji usiofaa kama vile uzito uliozidi, viriba tumbo, shinikizo la damu pamoja na kisukari. 
Amesema kasi ya ongezeko la magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza inapaswa kudhibitiwa kwa kuzingatia ulaji unaofaa na mtindo bora wa maisha. “Huu ni wakati wa kuangalia kwa pamoja kama jitihada zetu zinaleta matunda tunayotarajia.” 
Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua kuwa lishe bora ni msingi wa maendeleo ya Taifa letu hivyo, uwepo wao katika mkutano huo unaonesha umuhimu wa kuimarisha ushiriki wa kila sekta, kila mdau ikiwemo sekta binafsi kwa nafasi yake katika kupambana na aina zote za utapiamlo.  
Amesema ushiriki wa kila sekta ni wa muhimu kwa sababu hakuna sekta moja pekee inayoweza kuondoa tatizo la utapiamlo, pia ni vema kwa wadau hao wakajitathmini mmoja mmoja katika sekta zao kuona kama wanaelekea katika muelekeo sawa na mipango ya Serikali. 
“Kwa kuzingatia hilo, ofisi yangu imeweka utaratibu maalum wa kuratibu utekelezaji wa kazi za lishe nchini, ambapo kamati ya Kitaifa ya Usimamizi na Ushauri kuhusu masula ya lishe nchini yaani High Level Steering Committee on Nutrition imeundwa ili kusimamia utekelezaji wa azma hiyo.”  
Waziri Mkuu amesema kwamba watu wote wanatambua jitihada kubwa zilizowekwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau katika kupambana na matatizo ya lishe nchini, ambapo taarifa za wataalamu zinasema kuwa kwa sasa nchi inakabiliwa na aina mbili za utapiamlo yaani lishe duni na lishe iliyozidi au iliyokithiri.  
Amesema walengwa wakubwa wa lishe duni ni pamoja na watoto chini ya miaka mitano, wanawake walio katika umri wa kuzaa hususani wajawazito na wanaonyonyesha pamoja na vijana balehe (hususan wa kike). “Hii ni kwa sababu mahitaji ya virutubishi kwa ajili ya miili yao ni makubwa, ukilinganisha na ule unaohitajika na makundi mengine.” 
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa hafla ya kufungua mkutano wa tano wa wadau wa lishe wa kujadili na kutathmini utekelezaji wa afu za lishe leo jijini Dodoma. Mkutano huo unakauli mbiu ya "Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Lishe Bora ni msingi wa maendeleo yetu".

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  akizungumza wakati wa hafla ya kufungua mkutano wa tano wa wadau wa lishe wa kujadili na kutathmini utekelezaji wa afu za lishe leo jijini Dodoma. Mkutano huo unakauli mbiu ya "Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Lishe Bora ni msingi wa maendeleo yetu".

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Benilith Mahenge  akizungumza wakati wa hafla ya kufungua mkutano wa tano wa wadau wa lishe wa kujadili na kutathmini utekelezaji wa afu za lishe leo jijini Dodoma. Mkutano huo unakauli mbiu ya "Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Lishe Bora ni msingi wa maendeleo yetu".

  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Dkt. Vicent Asey akizungumza wakati wa hafla ya kufungua mkutano wa tano wa wadau wa lishe wa kujadili na kutathmini utekelezaji wa afu za lishe leo jijini Dodoma. Mkutano huo unakauli mbiu ya "Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Lishe Bora ni msingi wa maendeleo yetu".

 Mwakilishi wa kundi la vijana Rika Balehe ambaye pia ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Notre Dame ya jijini Arusha, Bi. Najma Mohamed akiwasilisha maoni yao kuhusu masuala ya lishe mbele wakati wa hafla ya kufungua mkutano wa tano wa wadau wa lishe wa kujadili na kutathmini utekelezaji wa afu za lishe leo jijini Dodoma. Mkutano huo unakauli mbiu ya "Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Lishe Bora ni msingi wa maendeleo yetu".

 Mtaalamu wa Lishe kutoka UNICEF, Mauro Brero akichangia mada wakati wa hafla ya kufungua mkutano wa tano wa wadau wa lishe wa kujadili na kutathmini utekelezaji wa afu za lishe leo jijini Dodoma. Mkutano huo unakauli mbiu ya "Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Lishe Bora ni msingi wa maendeleo yetu". Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...