Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) wamefunga siku tatu za uzibaji wa mivujo ya mabomba katika Mkoa wa Tabata na kufanikisha  kuziba mivujo 298 iliyokuwa sugu na mipya ikwia ni mikakati ya siku 100 ya Dawasa mya kuhakikisha wanaondoa tatizo hilo..

Zoezi hilo lililoanzia  Mkoa wa Dar es Salaam  katika maeneo ya Tabata zoezi limedumu kwa muda wa siku tatu na kufanikiwa kwa asilimia 85 kwenye kata zote 13.

Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji Mhandisi Aron Joseph amesema kuwa, zoezi hilo imeenda vizuri kwa mafundi wote kufanya kazi kwa ufanisi mzuri na kufanikisha kuziba mivujo yote 298 kwa asilimia 85 na tayari wameshakabidhi kwa Meneja wa Dawasa Mkoa wa Tabata.

Aron amesema,Tabata kulikuwa na changamoto kubwa sana ya Mivujo na wamefanikiwa kwa asilimia kuwa na kwa sasa wanahamia Ubungo kuanzia wiki ijayo na kuwataka mafundi waliofanikisha kuondoa changamoto ya mivujo Tabata kuwa ana imani watafanya kazi nzuri.

"Nina imani tunahamia Ubungo mafundi mtafanya kazi nzuri kama ya Tabata na hilo sina shaka, kwa takwimu Tabata kulikuwa kunaongoza kwa mivujo na hilo linatokana na kuwa na miundo mbinu chakavu ya muda nrefu na tumekabidhi kwa meneja wa Dawasa Tabata na tayari tumempa maelekezo kuwa mivujo yote itatakiwa kufanyika matengenezo ndani ya masaa 6,"amesema Aron.

Aliongezea na kusema, Dawasa mpya imeweka mikakati zaidi ya kuboresha miundo mbinu na  kuhakikisha ndani ya miaka mitatu miundo mbinu hiyo inabadilishwa na ili wananchi wasikose maji idara ya uzalishaji na usambazaji maji utahakikisha katika kipindi chote hicho watakuwa wanasimamia miundo mbinu hiyo ili kuondokana na uvujaji wa maji.
Meneja wa Dawasa Tabata Victoria Masele (kulia) akizungumza mbele ya Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji Mhandisi Aron Joseph na kuahidi kurekebisha mivujo yote ndani ya saa 6 kama alivyoagizwa baada ya kufanikisha kwa zoezi la uzibaji mivujo ndani ya Mkoa wake wa Tabata.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji Mhandisi Aron Joseph akizungumza na mafundi waliofanikisha kurekebisha kwa mivujo 298 katika Mkoa wa Tabata uliofanyika kwa siku tatu na kuwapongeza kwa kazi kubwa sana  walioifanya na kuwataka wajipange kwa Mkoa wa Ubungo.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...