Na: WFM,  Mjini Bali Indonesia
African Export Import Bank (Afreximbank) ya Misri, imeonyesha nia ya kuipatia Tanzania mkopo wa zaidi ya Shilingi trilioni moja (dola za Marekani zaidi ya milioni 500) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kipaumbele hasa ya miundombinu ya reli na kujenga vituo vya biashara (SEZ and Industrial parks).
Hayo yalibainishwa mjini Bali Indonesia, na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango baada ya Mkutano na Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel,  uliofanyika  wakati wa mikutano ya mwaka  ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ikiendelea.
Waziri Mpango, alisema kuwa Afreximbank imethibitisha kuwa ipo tayari kutoa mkopo wa  dola za Marekani milioni 125  (takribani Shilingi bilioni 285.9) kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Kimataifa  (SGR),  kipande cha Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma.
“Afreximbank wanania pia ya kutoa  dola milioni 400 (takribani Sh. Bilioni 914.9) ambazo wanaweza kutukopesha kwa ajili ya kugharamia miradi ya miundombinu itakayorahisisha biashara kati ya Tanzania na nchi jirani na Bara la Afrika kwa ujumla,  ili kuchochea kasi ya ukuaji wa biashara katika nchi hizo kwa lengo la kuondoa umasikini”, aliongeza Dkt. Mpango.
Alisema kuwa kwa kuwa tayari Tanzania ilikuwa na mkakati wa kufungua vituo vya biashara katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na mikoa mingine, suala la mkopo huo ni fursa kubwa kwa  maendeleo ya nchi, hivyo jambo hilo litafanyiwa kazi kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji  na Sekta Binafsi, ili Taifa liweze kunufaika na fedha ambazo benki hiyo ipo tayari kuzitoa.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akizungumzia miradi ya miundombinu ikiwemo ya Reli ya Kisasa kwa kiwango cha kimataifa, katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi, wakati wa Mkutano na Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel, uliofanyika Bali Indonesia, kulia ni Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga.
Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga, na Afisa Mwandamizi wa Wizara hiyo Bw. Elias Shosi, wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel, alipokuwa akizungumzia maamuzi ya benki yake kuikopesha Tanzania zaidi ya Shilingi trilioni moja wakati wa mkutano uliofanyika Bali, Indonesia.
Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga, na Afisa Mwandamizi wa Wizara hiyo Bw. Elias Shosi, wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel, alipokuwa akizungumzia maamuzi ya benki yake kuikopesha Tanzania zaidi ya Shilingi trilioni moja wakati wa mkutano uliofanyika Bali, Indonesia.
Meneja wa Afreximbank Kanda ya Afrika Mashariki Bw. Kudakwashe Matereke, akieleza jambo wakati wa Mkutano kati ya Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hawapo pichani), mjini Bali Indonesia wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel, wakipeana mkono baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao uliofanyika mjini Bali Indonesia wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...