Na Jumbe Ismailly SINGIDA 

MCHEZAJI mmoja wa timu ya soka ya Kijiji cha Iyumbu,tarafa ya Sepuka,wilayani Ikungi,Mkoani Singida,Mussa Kikumbu (20) amepoteza maisha na wengine 38 wamejeruhiwa vibaya baada ya gari aina ya kenta walilokuwa wakisafiria kwenda kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kata ta Mgungira kuacha njia na kupinduka.

Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wachezaji na washabiki waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida walisema ajali hiyo ilitokea Okt,07,mwaka huu saa tisa za alasiri wakati wakielekea kwenye mchezo wao wa kirafiki na timu ya kata ya Mgungira.

Mmoja wa majeruhi hao Emanueli Peter alisema waliondoka wakiwa watu 38 kwenye gari hilo na walipoanza safari askari mmoja wa kituo cha polisi Iyumbu alisema yeye hatapanda gari bali angekwenda na usafiri wake wa pikipiki.

Alifafanua majeruhi huyo alaiyelazwa katika wodi namba tatu katika Hospitali hiyo kwamba askari huyo alikuwa nyuma ya garai walilopanda akiendesha huku akionesha kila dalili za kuwa amekunywa kilevi huku dereva naye akiendesha mwendo kasi huku naye akiwa amelwa.
Kwa mujibu wa Peter inasemekana awali askari huyo alikuwa akitaka kumpita dereva wa gari ili aweze kutangulia lakini ilishindikana lakini baada ya muda alianza tena kuomba nafasi ili atangulie na alipopishwa ndipo ghafla alianguka chini.

Aidha majeruhi huyo aliweka bayana pia kwamba baada ya askari huyo kuanguka chini ndipo dereva wa gari walilopanda aliamua kumkwepaa ili asimkanyage na ndipo alipoingia kwenye korongo lililokuwa nje ya barabara na gari hilo kuanguka na kusababisha kifo cha mtu mmoja kati ya watu 39 waliokuwepo kwenye gari hilo.
FATUMA JISHIMU(19) aliyelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida pamoja na mwanaye MAARIAMU RAMADHANI(2) kufuatia ajali ya gari aina ya kenta iliyokuwa imewabeba wachezaji na washabiki Iyumbu FC waliokuwa wakienda kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya kata ya Mgungira FC.
PICHA Na.879 Ni MAGRETH SAWA (40) aliyelazwa katika wodi namba tatu hospitali ya Mkoa wa Singida akipatiwa matibabu kufuatia ajali ya gari aina ya kenta kucha njia na kupinduka katika Kijiji cha Iyumbu.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...