Asilimia 86 ya Wanawake na Asilimia 100 ya Wanaume mkoani Shinyanga wanasema kuwa umaskini wa familia ndio chanzo kikubwa cha mimba na ndoa za utotoni.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Shirika la Save The Children Bi. Neema Bwaira alipokuwa akitoa mada katika Mdahalo wa Kitaifa unaoendelea jijini Dar es Salaam kuhusu namana bora ya kupambana na ukeketaji, mimba na ndoa za utotoni.

Bi Neema ameongeza kuwa waliamua kufanya utafiti huu mdogo ili kupata kujua uelewa wa jamii ya mkoa wa Shinyanga katika suala la mimba na ndoa za utotoni.

Ameongeza kuwa utafiti huo umefanyika katika Wilaya za Kishapu, Kahama na Shinyanga Mjini ambapo umebaini  kuwa jamii bado haina uelewa kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni na bado vitendo hivi vimekumbatiwa kwenye mwamvuli wa mila na desturi.

“Kwa mujibu wa utafiti huu mdogo tulioufanya tumebaini kuwa umasikini na uelewa mdogo wa jamii kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni” alisisitiza Bi. Neema.

Bi Neema ameeleza kuwa Asilimia 11 ya wavulana na  Asilimia 9 ya wasichana  wanaamini kjuwa ni haki kwa mwanaume kumpiga mke wake na wanaamini kuwa mke anapomkosea mume ana haki ya kukubali kupigwa na mume na anakubaliana na hilo  ili kuifanya familia iendelee kukaa pamoja.
 Mwenyekiti wa Mdahalo ambaye pia ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinisa, Wazee na watoto Dkt. John Jingu (kulia) akiongoza Mdahalo wa kitaifa unaojadili namna bora za mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili hasa ukeketaji, Mimba na Ndoa za utotoni uliozinduliwa jana  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam katikati ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mtoto Bi Mwajuma Mwagwiza na kushoto ni Muongozaji wa Mdahalo kutoka Shirika la UNFPA Zanzibar Bi. Amina Kheri .
  Mwakilishi wa Shirika la Save The Children Bi. Neema Bwaira  akitoa mada katika Mdahalo wa kitaifa unaojadili namna bora za mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili hasa ukeketaji, Mimba na Ndoa za utotoni uliozinduliwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam.
 Mzee wa Mila kutoka Dodoma Chief Lazaro Masuma akitoa ushuhuda katika eneo analotoka kuhusu suala la ukeketaji, Mimba na Ndoa za Utotoni katika Mdahalo wa kitaifa unajadilia namna bora za mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili hasa ukeketaji, Mimba na Ndoa za utotoni uliozinduliwa jana  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa Ngariba Mstaafu Bi.Rahel Masagara akitoa ushuhuda akisisitiza wazazi kutimiza wajibu na majukumyu yao kwa watoto hasa wa kike kuhusu suala la ukeketaji, Mimba na Ndoa za Utotoni katika Mdahalo wa kitaifa unaojadili namna bora za mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili hasa ukeketaji, Mimba na Ndoa za utotoni uliozinduliwa jana  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa Maendeleo na Ustawi wa mtoto nchini wakifuatilia Mdahalo wa kitaifa unaojadili namna bora za mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili hasa ukeketaji, Mimba na Ndoa za utotoni uliozinduliwa jana  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...