Na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha
Jeshi la Polisi mkoani hapa limemkamata kijana mmoja jina linahifadhiwa mkazi wa Daraja Mbili halmashauri ya jiji la Arusha akiwa na kilogramu 207 za dawa ya kulevya aina ya Mirungi.

Akitoa taarifa hiyo mapema leo ofisini kwake, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi alisema kwamba, mtuhumiwa huyo alikamatwa jana saa 6:00 Mchana akiwa anatokea mpakani mwa mkoa wa Kilimanjaro kuingia mkoa wa Arusha aliamua kutumia mbinu mpya ya usafirishaji wa dawa hazo kwa kujipachika katikati ya msafara wa magari yaliyokuwa yanakwenda msibani.

Kamanda Ng’anzi alisema kwamba Jeshi hilo lilipata taarifa juu ya uwepo wa mtu huyo aliyekuwa anasafirisha Mirungi kwa kutumia gari ndipo walipowapeleka askari haraka katika eneo la Kikatiti wilayani Arumeru na kuweka mtego.

“Wakiwa katika eneo hilo baada ya muda askari hao waliona gari aina ya Suzuki Escudo rangi ya Kijivu lenye namba za usajili T 505 CNC likiwa katikati ya msafara wa magari yaliyokuwa yanaelekea msibani lakini kwa umahiri mkubwa walilibaini ndipo wakalizuia”. Alifafanua Kamanda Ng’anzi.

Kamanda Ng’anzi alisema kwamba baada ya kufanya upekuzi waligundua kuwepo kwa dawa hazo yaliyohifadhiwa nyuma ya “boot” yakiwa yamehifadhiwa kwenye viroba tofauti tofauti vyote vikiwa na uzito wa kilogramu 207.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) ramadhani Ng'anzi akiwaonyesha waandishi wa habari viroba mbalimbali vya dawa za kulevya aina ya Mirungi vilivyokuwa vinasafirishwa kwa kutumia gari aina ya Suzuki Escudo lenye namba za usajili T 505 CNC. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Gari aina ya Suzuki Escudo rangi ya kijivu lenye namba za usajuili T. 505 CNC ambalo lilikamatwa eneo la Kikatiti wilayani Arumeru likiwa na viroba vya dawa za kulevya aina ya Mirungi yenye uzito wa Kilogramu 207.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng'anzi akionyesha baadhi ya pikipiki zilizokamatwa kutokana na msako ambazo zilikuwa zinatumiwa na wahalifu waliokuwa wanapora pochi kwa watembea kwa miguu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...