Frank Mvungi- MAELEZO
MKUU wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge, ameongoza mkutano
wa majadiliano ya Baraza la Biashara la mkoa huo ili kupitia na kuhakiki
mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili usaidie
kukuza ushiriki wa sekta binafsi na kuchochea ukuaji wa sekta zinatoa ajira kwa
wananchi walio wengi kama kilimo.
Akizungumza na wajumbe wa baraza hilo leo Jijini Dodoma na wadau wengine, Dkt. Mahenge amesema kuwa,
mkutano huu una lengo la kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma
na sekta binafsi ngazi ya Mikoa na Wilaya.
“Tunategemea
utakuwa rejea thabiti kwa viongozi na watendaji ambao wamekuwa wakibadilika
mara kwa mara kutokana na uteuzi au chaguzi”. Alisisitiza Dkt. Mahenge
Akifafanua
zaidi, mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma amesema mkutano huo wa majadiliano una lengo
la kuhakikisha ushiriki wa sekta binafsi unaongozeka ili kuchochea maendeleo ya
mkoa na taifa.
Aliongeza
kuwa, majadiliano hayo yatasaidia kutatua changamoto zinazojitokeza mara kwa
mara ambazo zimekuwa zikifubaza upatikanaji wa fursa za kiuchumi na kijamii na
yanategemewa kutoa ufumbuzi wa changamoto hizo kwa kuzingatia maandalizi
ya majadiliano, kanuni za majadiliano na utekelezaji baada ya majadiliano.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge akifungua mkutano wa kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi uliofanyika leo Jijini Dodoma.
Mhadhiri kutoka Chuo kikuu Mzumbe Prof. Honest Ngowi akiwasilisha rasimu ya mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi wakati wa kikao cha kujadili muongozo huo leo Jijini Dodoma.
Sehemu ya wakuu wa Wilaya wa mkoa wa Dodoma wakifuatilia mkutano wa kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi uliofanyika leo Jijini Dodoma.
(Picha
zote na MAELEZO)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...