Benki ya NIC Tanzania, leo imeitambulisha  huduma ya malipo ya bima kuwawezesha watejawetu ambao ni wanachama wa shirika la Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA)  kulipia michango ya bima kidog kidogo.

“Tunaona uwezo mkubwa sana kwenye magari ya usafirishaji abiria na pia ya mizigo. Huduma hii mpya ya bima inatupa nafasi ya kipekee kukuza biashara yetu kwa upande mmoja na kwaupande mwingine kuwarahishia malipo wateja wetu,” bwana Rahim Kanji, Meneja Mkurugenzi  wa NIC kitengo cha biashara alisema.

“Kusisitiza umuhimu wa huduma hii, tumeweka timu maalamu kusimamia utoaji wa huduma hii kwa wamiliki wa basi nchini kote,” aliendelea kusema.

 “Mkutano huu na TABOA ni hatua muhimu kama benki ya NIC tukiwa tunaendelea na  mchakato mzima wakutoa huduma bora kwa wateja wetu na watanzania kwa ujumla ambazo zina boresha maisha yao. Benki yetu haiachi kutafuta namna za kueendelea kuboresha na kuzindua huduma mbali mbali zinazo timiza mahitaji ya aina tofauti,” aliongezea.

Mnamo mwaka wa 2009, Benki mama ya NIC (NIC Bank Group) ilinunua hisa katika benki ya Savings and Finance (S&F) Commercial Bank na kuibadilisha kwa mafanikio makubwa kuwa benki ya NIC Tanzania. NIC Bank Group ndio benki mama ya benki ya NIC Kenya, ambayo inamaffanikio makubwa sana Kenya ambapo ni benki ya 7 kwa ukubwa wa wanahisa naya 9 kwa ukubwa wa rasilimali.

NIC Bank Group imeendelea kukuwa kwakiasi kikubwa kadiri miaka inavyo enda na hii ikiwa sambamba na mpango wake endelevu wa  “Kujenga mafanikio kwa pamoja” Benki ya NIC Tanzania inaweka msisitizo mkubwa kukuwa na wateja wake wenye biashara ndogo na zakati, biashara za nyumbani, wahitimu, na wakurugenzi wa mashirika makubwa.
Meneja wa biashara benki ya NIC,Rahim Khanji (kushoto) akijibu maswali  ya wanachama wa shirika la Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) baada ya kutambulisha huduma ya malipo ya bima ya awamu kwa wamiliki wa mabasi,ambapo itawawezesha wamiliki hao kulipia michango ya bima kidogo kidogo kupitia benki hiyo.
Meneja msaidizi masoko wa benki ya NIC,Natasha Cathles (kushoto) akiwafafanulia wanachama wa shirika la Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) namna ya kujiunga na huduma ya malipo ya bima ya awamu kwa wamiliki wa abasi,ambapo itawawezesha wamiliki hao kulipia michango ya bima kidogo kidogo kupitia benki hiyo.
Wamiliki wa Mabasi ambao ni wanachama wa TABOA wakiwa kwenye kikao wakati wa  kutambulisha huduma ya malipo ya bima ya awamu kwa wamiliki wa mabasi,ambapo itawawezesha wamiliki hao kulipia michango ya bima kidogo kidogo kupitia benki hiyo.
Wafanyakazi wa NIC Bank wakiwa katika picha ya pamoja


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...