BENKI ya NMB imekabidhi msaada wa vitabu na udhamini wa jezi, mabegi ya michezo na mipira kwa kituo cha vijana cha Don Bosco Upanga cha jijini Dar es Salaam kinachomiliki timu mbili za mchezo wa mpira wa kikapu kwa wanaume na wanawake ambazo ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa mchezo huo.

Msaada huo na udhamini wa vifaa hivyo kwa kituo hicho kinachosaidia vijana umegharimu kiasi cha shilingi milioni 15, ambapo akikabidhi Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite alisema benki hiyo itaendelea kuchangia katika shughuli za kusaidia jamii pamoja na kuinua michezo nchini.Akifafaanua katika ufadhili huo, Bw. Ngingite alisema ufadhili huo umejumuisha vitabu mbalimbali kwenye maktaba ya kituo cha Don Bosco Upanga pamoja na vifaa vya michezo vitakavyotumiwa na timu ya mpira wa kikapu wanaume ya Savio na timu ya mpira wa kikapu wanawake ya Lioness zote zikilelewa na kituo hicho.

Alisema NMB imetenga takribani shilingi bilioni moja ikiwa ni maalum kusaidia shughuli za kijamii ikiwemo sekta za afya, elimu na majanga endapo yanaikumba jamii. Alisema michezo mbali na kuwa ajira kwa vijana pia inawajenga kiafya na kuwawezesha kufanya vizuri hata kwenye elimu.Timu za mpira wa kikapu za Savio na Lioness ambazo zipo chini ya kituo cha Don Bosco Ukonga ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa mchezo huo, na kwa udhamini wa NMB wao wamenufaika kupata jezi za kisasa, mipira ya mchezo huo pamoja na mabegi maalum ya michezo kujiandaa na mashindano aanuai.

Kwa upande wake Mlezi wa Kituo cha Don Bosco Upanga, Padre Michael Muia aliishukuru Benki ya NMB kwa ufadhili na msaada walioutoa kwa kituo hicho na kuahidi wataitumia vizuri iwe chachu ya mafanikio zaidi kwa vijana.

Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite (wa pili kushoto) akimkabidhi Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa moja ya jezi zilizotolewa na NMB kwa ajili ya timu za mpira wa kikapu za Savio (wanaume) na Lioness (wanawake) kama sehemu ya udhamini wa timu hizo ambazo ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam. 
Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite (wa pili kushoto) akimkabidhi Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa moja ya mabegi yaliyotolewa na NMB kwa ajili ya timu za mpira wa kikapu za Savio (wanaume) na Lioness (wanawake) kama sehemu ya udhamini wa timu hizo ambazo ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam. 
Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite (wa pili kushoto) akimkabidhi Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa moja ya mipira iliyotolewa na NMB kwa ajili ya timu za mpira wa kikapu za Savio (wanaume) na Lioness (wanawake) kama sehemu ya udhamini wa timu hizo ambazo ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...