BENKI ya TIB Corporate washeherekea wiki ya huduma kwa wateja kwa kutembelea wateja wake.

Leo Oktoba 11 benki hiyo wamewatembelea Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Shirika la Bima la Taifa (NIC) ikiwa ni kwaajili ya kuwashukuru pamoja na kujitadhimini jinsi ya utoaji wa huduma kwa wateja wao.

Akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amewashukuru wafanyakazi wa benki hiyo kwa kuwaona wamhimu katika kuendeleza gurudumu serikali ya viwanda hapa nchini kwa utunzaji wa fedha.

Nae Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga amewashukuru kwa kuona nchango wa shirika hilo pia pia amewaasa kujitangaza zaidi ili kuondoa mkanganyiko uliopo katika jina la benki hiyo.


Mkurugenzi mkuu wa benki ya TIB Corporate Frank Nyabundege akizungumza na wafanyakazi wa beki ya TIB Corporate jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Oktoba.
Meneja kitengo cha sheria wa benki ya TIB Corporate Berina Rugaiyamu
 akimkabidhi ua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa baada ya kutembelewa ofisini kwake na wafanyakazi wa TIB Corporate jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru wateja wa benki hiyo katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa  akifurahia jambo mara baada ya kutembelewa na wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate jijini Dar es Salaam leo.
meneja wa rasilimali watu  wa benki ya TIB Corporate Irene Ungani Kyara  akiwamkabidhi Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga mara baada ya kumtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kwaajili ya kushaherekea pamoja na kujitathimini katika wiki ya huduma kwa wateja ambapo benki hiyo imeadhimisha mwaka huu kwa kuwatembelea wateja wake mahali walipo.
Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga mwenye miwaniakizungumza na wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate jijini Dar es Salaam leo  ikiwa ni adhima ya benki hiyo kuwatembelea wateja wake.


Picha za pamoja za wafanyakazi  wa benki ya TIB Corporate.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...