*kutua nchini Oktoba 10 mwaka huu.

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

MCHEZAJI wa zamani wa timu ya Taifa ya Cameroon na Barcelona Samuel Eto'o anatarajia kuja nchini  kwa ajili ya uzinduzi wa  mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira  wa soka  aina ya 5-A-side utakaojengwa Oysterbay jijini Dar es salaam. Eto'o anakuja nchini kwa mualiko wa kampuni ya bia ya Tanzania (TBL) kupitia bia ya Castle Lager na atawasili Oktoba 10 mwaka huu.
 Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Meneja wa bia hiyo Pamela Kikuli amesema kuwa nyota huyo atashiriki katika uzinduzi  huo  wa uwanja maalumu wa soka linaloshirikisha wachezaji kumi (watano kila upande) maarufu kama ‘5-A-Side soccer’ katika eneo la Oysterbay  mkabala na jengo la Coco Plaza, jirani na fukwe za Coco.
 
Ameeleza kuwa lengo la kumleta nguli huyo wa soka barani Afrika ni kuongeza hamasa ya soka kwa wanamichezo wenye vipaji kujitokeza kushiriki katika kabumbu.
Pia amesema kuwa kama kampuni wataendelea kushiriki katika shughuli za kijamii katika kuleta maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Msemaji ya klabu ya Simba  amesema kuwa urafiki unasimama hasa katika wakati wa kuliwakilisha taifa na amewataka mashabiki wa klabu za Simba na Yanga kujitokeza kwa wingi.

Dismas Ten msemaji wa klabu ya Yanga amesema kuwa ujio wa Eto'o nchini ni heshima kubwa kwa nchi na soka kwa ujumla hivyo wananchi hasa wapenda soka ni bora wakajitokeza ili kuweza kumfahamu nguli huyo wa mpira wa miguu.

Samuel Eto'o  anayesakata kabumbu huko Qatar anatarajia kuwasili katika uwanja wa Mwalimu Nyerere Oktoba 10 na siku ya Alhamisi atatembelea mradi huo wa ujenzi wa uwanja hicho na kushiriki mazoezi na vijana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...