Katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Kata ya Mtoni Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam Ndg. Humphrey Polepole Katibu Mwenezi wa CCM amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitawachukulia hatua kali Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wanaotokana na CCM wasio soma mapato na matumizi kwa wananchi kwa mujibu wa Sheria.

Akifafanua suala hilo Ndg. Polepole ameeleza kuwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa wa Mwaka 2019 CCM inahitaji watu watakao kuwa Viongozi wa wananchi kupitia CCM wenye sifa nzuri kwenye mitaa yao, amekemea suala la urafiki, undugu na upangaji wa safu katika mchakato wa kuwapata viongozi wa wananchi na amewataka Viongozi wa CCM na Viongozi wa Serikali ngazi zote kuwa na ushirikiano kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi kwa haraka.

“Wapo wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa CCM wasio soma mapato na matumizi…watu jeuri… wanafanya nini kwenye Chama chetu..? hawa hatuendi nao hadi mwaka 2019…kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwakani tunataka watu wenye sifa nzuri” amesisitiza Ndg. Polepole

Aidha Ndg. Polepole ametumia mkutano huo kusisitiza kuhusu suala la  Viongozi wa Serikali hususani wakuu wa Wilaya kuendeleza utaratibu wa kusikiliza wananchi na utolewaji wa mikopo ya Halmashauri bila riba kwa makundi ya kina Mama, Vijana na Watu wenye ulemavu ili kuwawezesha wananchi kiuchumi na kutatua shida na changamoto zao kwa haraka.

Huu ni muendelezo wa vikao vya ujenzi na uimarishaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuhakikisha dhana ya Chama imara, Serikali imara inadhihirika.
 Katibu Mwenezi wa CCM Ndg. Humphrey Polepole akizungumza Katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Kata ya Mtoni Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...