Na Khadija Seif,globu ya jamii

RAIS mpya wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam(DSJ) Esther Amandus ameapishwa rasmi huku akitumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa wote walioshiriki uchaguzi huo.

Sherehe za kuapishwa kwa Rais huyo pamoja na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali umefanyika leo chuoni hapo.Pia wanafunzi wengine waliopo na wale waliowasoma chuoni hapo walishiriki tukio hilo.

Akizungumza chuoni hapo Amandus ametoa shukrani kwa kila mmoja aliyeshiriki kwenye uchaguzi kwani wote walifanya uchaguzi wa haki na demokrasia .Amesema anatarajia kufanya kazi na wanafunzi wote wa DSJ katika kuzisikiliza shida ,kero na mahitaji yao ili kutetea maslahi ya chuoni hicho.Pia ameshukuru uongozi chuoni hapo na kuwaomba kushirikiana nao bega kwa bega katika kukiletea maendeleo chuo .

Amesisitiza chuo cha DSJ kimetoa waandishi mahiri ambao wako kwenye tasnia ya habari nchini akiwemo Salum kikeke,Charles Hillary na wengine wengi ambao wameleta mapinduzi kwenye habari na kuwa mifano ya kuigwa kwa mazuri ambayo wanafanya kama kutangaza na kuripoti taarifa kwenye lafudhi zinazoeleweka.

Hata hivyo licha ya kuwepo kwa mafanikio mengi chuoni hapo pia changamoto hazikosekani basi kwa pamoja wakishirikiana na wanafunzi ambao wapo kwa muda mrefu chuoni hapo wataweza kuleta mabadiliko makubwa.
Ametoa rai kwa wanachuo waimarishe umoja na mshikamano ili kukuza demokrasia na utawala bora 
chuoni hapo.

Aidha Rais huyo mpya ameahidi kuyafanyia kazi mapendekezo aliyoyatoa Mkuu wa chuo Joachim Rupepo, kupitiwa upya na kurekebishwa kwa Katiba ya Serikali ya Wanafunzi (DASJOSO).

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Serikali ya mpito Darbina Amani amewashukuru wanafunzi wote chuoni hapo kwa ushirikiano walioonesha kipindi chote walichokua madarakani na kuomba radhi kwa wote ambao waliwakwazwa .

Amani amewataka wanafunzi kuonesha matatzo uadilifu,hekima n heshima juu ya uongo huo mpya ili Kule mabadiliko mengi .

Rais mpya wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) Esther Zalamulla akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 12, 2018 jijini baada ya kuapishwa rasmi 

Rais mpya wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam(DSJ) Esther Zalamulla (kulia) wakipongezana na Waziri wa Michezo mstaafu Makame Mohamed leo Oktoba 12, 2018 jijini baada ya kuapishwa rasmi 

Picha ya pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chuo hicho wakiwa na Mkuu wa Chuo Joachim Rupepo(wa pili kushoto aliyekaa)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...