CHAMA  cha  walimu   Tanzania (CWT)  wilaya ya  Kilolo  mkoani Iringa  kimetoa  bati   500  zenye  thamani  ya  zaidi ya  shilingi milioni 8.5 kwa   mwalimu  mstaafu  25  kama  sehemu ya  kuwaaga na  kuwapongeza kwa  utumishi  bora katika  kazi  hiyo ya  ualimu .

Akikabidhi   bati  hizo jana  wakati wa  hafla  fupi ya  kuwaaga  walimu  hao  mgeni  rasmi katika  hafla  hiyo afisa   utumishi  wa  Halmashauri ya  wilaya ya  Kilolo   Josephat  Kayombo   pamoja na  kupongeza   CWT wilaya ya   Kilolo  kwa  kutambua  mchango  wa   walimu   wenzao  ambao  wamestaafu  bado  alitoa  wito  kwa  walimu   waliopo kazini  kuendelea kujituma  kufanya kazi hiyo na  kujiepusha  na  utovu  wa  nidhamu .

Kayombo  alisema   serikali  imeendelea  kuwajali  watumishi  wote  wa umma  wakiwemo  walimu na kuendelea  kulipa  stahiki  zao ambazo  wamekuwa  wakizidai hivyo  ni lazima  kwa  watumishi hao kutimiza  majukumu yao  kwa  ufanisi na  kuepuka   kuonyesha  utovu wa  nidhamu  na  jeuri  pale  mwajili  ambapo amua  kumpangia kituo kipya  cha kazi .

"  Walimu  ni  kielelezo  tosha  kwa  jamii na hakuna yeyote  anayeweza  kujisifu  kwa  mafanikio yake  bila  kutambua  mchango wa  mwalimu   hivyo ni vema  walimu  kwa  umuhumu  wenu  huo kuendelea   kulenda   heshima  yenu kwa   kuonyesha  nidhamu na  kuzingatia  kanuni  na  taratibu za  kazi  na  kujiepusha  kuwa  na  nidhamu  mbovu "  alisema  Kayombo 

 Pia  alisema    kwa  kuwa  serikali  imeendelea  kuwalipa  mafao  yao   wastaafu    ni  vema  walimu    wastaafu  kuwa makini na  wimbi la  matapeli  ambao  wamekuwa  wakizunguka katika vijiji mbali mbali  vya  wilaya ya  Kilolo  na  kuorodhesha majina ya  walimu  wastaafu  kwa  lengo la  kuwatapeli   mafao  yao  ya  ustaafu .

Alisema  kuwa  kiasi cha  fedha  ambacho  wanakipata  baada ya  kustaafu  kinaweza  kuja  kuwa msaada  mkubwa  kwao mbele ya  safari    hivyo  umakini unahitajika  kwa  kuwaepuka  matapeli  hao.
Afisa utumishi  wilaya ya  Kilolo  mkoani Iringa Joseptah kayombo (kulia)  akiwa na  viongozi wa chama cha walimu Tanzania (CWT)  wilaya ya  Kilolo wakiwakabidhi bati  walimu  wastaafu 25  kila  mmoja bati 20.
 Viongozi wa CWT  Kilolo (kulia)  wakiwakabidhi walimu wastaafu 25 zawadi ya bati 20 kila  mmoja .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...