Na Mwandishi wetu- Uyui
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe. Gift Msuya amewatembealea na kuwapa pole wananchi walioathirika na uvamizi wa Tembo katika Kijiji cha SawMill Kata ya Migiri.
Akizungumza  na wananchi hao mara baada ya kuwatembelea na kuwafariji amesema kuwa ameshawaagiza Askari wanyamapori kufika katika kijiji hicho na kuwaondosha tembo hao ili wasiendele kuleta madhara katika eneo hilo ikiwemo kuharibu mali na kudhuru wananchi .
“Jukumu la Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama na wanaendelea na shughuli zao za uzalishaji kama kawaida ndio maana nimewaagiza askari wanyamapori kufika hapa mara moja na kuwaondosha tembo hawa” ; Alisisitiza Msuya
Akifafanua amesema kuwa tembo hao ambao idadi yao haikufahamika waliingia katika kijiji hicho na kuanza kuharibu mazao ya chakula yaliyokuwa yamehifadhiwa na wananchi hao katika vihenge.
Pia aliwataka wananchi katika maeneo hayo kuishi kwa tahadhari kwa kutoa taarifa haraka pale watakapoona wanyama hao wameingia katika makazi yao ili Serikali ichukue hatua stahiki kwa  haraka kuepusha maafa.
Tembo hao ambao idadi yao haikufahamika mara moja walivamia makazi ya watu usiku wa kumakia tarehe 15 Oktoba na kusababisha uharibifu wa wa mazao ya chakula yaliyokuwa yamehifadhiwa na wananchi hao.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift  Msuya  akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa wananchi walioathirika na uvamizi wa tembo katika kijiji  SawMill Kata ya Migiri Wilayani humo.  (Picha zote na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...