Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro(Mb.) na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe wamekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani Bi. Inmi Patterson. Katika mazungumzo yao Bi. Patterson alitumia firsa hiyo kujitambulisha na kuwampongeza kwa kuteuliwa kuwa Naibu Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo. Aidha, Dkt Ndumbaro amemuhakikishia Bi. Patterson kumpa ushirikiano wa karibu katika kutekeleza majukumu yake. Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam Tarehe 16/10/2018
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damasi Ndumbaro (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. Sarah Cooke, katika Mazungumzo hayo Mhe. Cooke ametumia fursa hiyo kujitambulisha na kuwapongeza Mhe. Ndumbaro pamoja na Katibu Mkuu Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (hayupo pichani). Aidha, Balozi Cooke alitumiafursa hiyo kumweleza Dkt. Ndumbaro pamoja na Dkt. Mnyepe kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza ni wa muda mrefu sana ambapo nchi hizi mbili zinashirikiana katika sekta mbalimbali za kukuza uchumi. Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam Tarehe 16/10/2018
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damasi Ndumbaro (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uganda nchini Mhe. Richard T. Kabonero. Katika Mazungumzo hayo Mhe. Kabonero ametumia fursa hiyo kujitambulisha na kumpongeza Mhe. Ndumbaro pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (hayupo pichani).
Aidha, Balozi Kabonero alitumiafursa hiyo kumweleza Dkt. Ndumbaro pamoja na Dkt. Mnyepe kuwa mahusiano kati ya Tanzania na Uganda ni ya muda mrefu, ambapo kutokana na mahusiano mazuri kati ya nchi hizi imepelekea Serikali ya Uganda kuamua kupitisha ujenzi wa bomba la mafuta tanzania, ambapo ujenzi huo utazalisha fursa mbalimbali na kukuza vipato vya wananchi wa pande zote mbili pamoja na kukuza uchumi baina ya mataifa hayo mawili.
Kwa upande wa Dkt. Ndumbaro amemuhakikishia Balozi Kabonero kumpatia ushrikano wa kutosha wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya kuiwaikilisha Taifa lake hapa nchini, Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam Tarehe 16/10/2018.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...