WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaweka mikakati madhubuti kwa lengo la kuimarisha matumizi ya fukwe kama sehemu ya kivutio cha utalii ili kongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini na kutengeneza ajira kwa wananchi sambamaba na kukuza uchumi wa Taifa.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Oktoba 12, 2018) wakati alipomuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye ufunguzi wa onesho la Kimataifa la Utalii la Swahili International Tourism Expo, katika  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar ES Salaam.

Onesho hilo linalofanyika kwa siku tatu nchini linahudhuriwa na wafanyabishara wakubwa wa utalii takriban 170  kutoka nchi mbalimbali duniani pamoja na wauzaji wa bidhaa za utalii takriban 300 kutoka ndani na nje ya nchi.

Waziri Mkuu amesema sekta ya utalii nchini inachangia zaidi ya asilimia 25 ya mauzo yote ya nje na takriban ajira 1,500,000, ambapo kati ya ajira zote za moja kwa moja na zile ambazo si za moja kwa moja.

Amesema kutokana na juhudi za utangazaji wa vivutio vya utalii nchini unaoratibiwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), wageni wengi maarufu duniani wanakuja kuona vivutio hivyo wakijua kwamba Tanzania ni nchi ya amani, yenye utulivu na Watanzania ni watu wakarimu. 

Amsema kati ya wageni hao waliokuja hapa nchini kwa mwaka huu ni pamoja Rais Mstaafu wa Marekani, Bw. Barack Obama aliyekaa siku nane; Rais wa Uswisi Bw. Alain Berset aliyekaa siku 10 pamoja na mchezaji wa golf mstaafu kutoka Marekani, Bw. Jack Nicklaus.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wadau wa utalii, kwenye ufunguzi wa maonesho ya Swahili International Tourism Expo, yaliyofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere Dar es salaam, Oktoba 12, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Thomas Mihayo, wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Dar es salaam, kufungua maonesho ya Swahili International Tourism Expo Oktoba 12, 2018, katikati ni Naibu Waziri wa maliasili na Utalii Josephat Hasunga , kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la ndege Tanzania (ATCL) Ladiclaus Matindi, alipotembelea mabanda, kwenye ufunguzi wa maonesho ya Swahili International Tourism Expo, yaliyofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere Dar es salaam, Oktoba 12, 2018, kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, Naibu Waziri wa maliasili na Utalii Josephat Hasunga, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Thomas Mihayo. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia bidhaa za Tanzania zinazotolewa ndani ya ndege ya ATCL, kwenye ufunguzi wa maonesho ya Swahili International Tourism Expo, yaliyofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere Dar es salaam, Oktoba 12, 2018, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la ndege Tanzania (ATCL) Ladiclaus Matindi na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Thomas Mihayo. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...