Na Karama Kenyunko Globu ya jamii

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Halotel inakusudia kuwekeza dola za kimarekani (USD) 700 katika sekta Umma na  mawasiliano nchini ikiwa na malengo ya kuwafikia wateja zaidi ya milioni Sita katika kipindi cha miaka mitano toka kuanzishwa kwake.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Halotel Tanzania, Nguyen Van Son, amesema hayo leo Oktoba 16,2018 wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu ya Halotel yaliyofanyika katika ofisi zao.

Son amesema, pamoja na mipango hiyo ya kuwekeza, kampuni hiyo pia imekusudia kuboresha zaidi Huduma ya utumaji wa pesa kwa njia ya mtandao, 'Halopesa' kwa ajili ya Wateja binafsi, mashirika na serikali kwa ujumla.

 "Mpaka sasa tunatimiza miaka mitatu Halotel inefanya uwekezaji wa dola za kimarekani (USD) 500 ikiwa ndio kampuni inayoongoza kwa kwa kuwekeza miuondombinu ya mawasiliano katika sehemu mbalimbali nchini inayowafikia asilimia 95 ya wananchi wote ikiwa n vituo 4400 vya kupokea mawasiliano" amesema Son.

Kampuni hiyo imepanga kuimarisha mtandao wake wa 4G ili kuwafikia Wateja wengi zaidi hadi wale walioko pembezoni mwa miji na kuwapa gharama nafuu za mawasiliano ambapo mpaka sasa Wateja zaidi ya milioni tatu na wengine zaidi ya milioni moja waliojiunga na Halopesa.

Ameongeza, kuwa kupitia Huduma hio wanaamini watakuwa wameisaidia serikali na taasisi zote za kibiashara kuendeleza Utoaji wa Huduma zao kwa ufanisi ukizingatia Halotel imekuwa ikishiriki katika shughuli mbali mbali za kijamii zinazoliwezesha taiga kufikia malengo yake mbali mbali

Naibu mkurugenzi mkuu wa Halotel Nguyen Van Son akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusheherekea miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake hapa nchini kulia ni  katibu wa  kampuni hiyo Nguyen Thi Thuy Linh.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halote, Mhina Semwenda kulia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuadhimisha miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake hapa nchini. kushoto ni Naibu mkurugenzi Mkuu wa Halotel, Nguyen Van Son.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Naibu mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son jijini Dar es Salaam leo Oktoba 16.Picha na Avila Kakingo,Globu ya jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...