Na Khadija Seif, Blobu ya Jamii
Mwanamuziki wa kike nchini anaejulikana kwa jina la Hawa  aliyeshirikishwa kwenye wimbo wa "Nitarejea" wa Mwanamuziki Naseeb Abdul 'Diamond platinumz' amefanikiwa kupata vipimo vya awali nchini India.
Hawa ambaye hivi karibuni alikua akiomba msaada kwa watu mbalimbali  ikiwemo kwa Diamond ili aweze kupata matibabu ya ugonjwa ambao ulikua ukimsumbua muda mrefu huku wengi wakimtupia lawama kuwa amejiingiza Kwenye ulevi wa kupindukia.
Akithibitisha hayo Meneja wa Daimond Platinum, Hamis Tale maarufu kama Babu Tale ameeleza kuwa wamefika salama nchini India na kufanikiwa kupata vipimo vya awali.
Tale ameweka wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika 
"Asante Mungu tumefika salama India na tumefanya vipimo vyote upya salama na jibu lililotoka kwa wataalamu kwa asilimia 95% awajaona tatizo linalohusiana na ini kwa mgonjwa ila ni moyo ndio uliokua unapelekea mgonjwa kujaa maji mwilini ivyo basi kutaitajika kufanyika upasuaji mkubwa ambao utakua na uangalizi mkubwa wa wataamu then wametuakikishia baada ya hapo mgonjwa atapata nafuu na inawezekana izo 5% zilizobaki itakua poa na tatizo la ini alitokuwepo kikubwa tunaomba mtuombee dua na msiache kumuombea pia @diamondplatnumz apatenguvu ya kuendela kumsaidia kwa maana kutoa ni moyo. Kikubwa sana naomba tumuombee Hawa coz anaingia kwenye upasuaji mkubwa na hii ni atua ya yeye kua salama. Mungu tusimamie"

Hivyo basi tale amesema kuwa Hawa amefanya kipimo cha moyo nakugundulika kuwa ndio chanzo kilichokua kikipelekea mwili kujaa maji.

Wataalamu wanaendelea kuhakikisha Hawa anapata matibabu na taratibu zinaendelea vizuri ili aweze   kufanyiwa upasuaji mkubwa ambao utahitaji uangalizi sana. Pia Meneja huyo ameshukuru sana juhudi ambazo zinaonyeshwa kwa msanii daimond kwa kumsaidia mwana Dada huyo ili kuhakikisha anarudi katika hali yake ya kawaida na kuwasihi watu kumuombea dua sana katika kipindi hiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...