Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akisoma kijarida cha Hifadhi ya Taifa ya Saaadani alipotembelea banda la maonesho la Hifadhi hiyo katika Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Oktoba 20,2018. Kulia ni Mhifadhi Utalii wa Saadani Bi. Apaikunda Mungure.

Hifadhi ya Taifa ya Saadani kupitia Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo limetangaza ofa Watanzania na wasio Watanzania kutembelea hifadhi hiyo kuanzia Oktoba 25, 26 na 27 mwaka huu kujionea vivutio mbalimbali vya Utalii.

Akizungumza Mhifadhi Utalii, Hifadhi ya Saadani, Bi. Apaikunda Mungure amesema ofa hiyo ni maalum kwa msimu huu wa tamasha la Sanaa Bagamoyo  ambapo kwa kiasi cha Tsh. 91,000   ni gharama kwa Raia wa Tanzania pamoja na Afrika Mashariki huku wageni kutoka nje ya Afrika Mashariki hao watalipia US$120 tu.

“Ofa hii itanda kwa muda wa siku tatu. Oktoba   25, 26 na 27. Wageni wataenda Saadani na kurudi hapa Bagamoyo. Kwa kiasi hicho cha Tsh. 91,000 inajumlisha usafiri wa magari ya Kitalii, usafiri wa kuzunguka na boti kwenye makutano ya Mto Wami na bahari ya Hindi.

Pia watapata kifungua kinywa, chakula cha mchana na vinywaji na kutembelezwa kwa safari za kuangalia wanyama na magari” alieleza  Bi. Apaikunda Mungure.

Ameongeza kuwa kwa familia itakayokuwa na motto atamlipia Tsh. 71,000.

Saadani  ni hifadhi ya kipekee ambapo Nyika na bahari  vinakutana pamoja. Ndani ya hifadhi hiyo ina aina mbalimbali za wanyama pori, fukwe ya bahari ya hindi.

Iko katika mkoa wa Pwani na Tanga

Watanzania ambao wapo Bagamoyo na miji jirani ya Dar es Salaam ni fursa ya kujitokeza kwenda kujionea Utalii wa ndani wenye kila aina ya vivutio vya Wanyama na safari zitakuwa kila siku kwa wageni kuanzia saba ambao wao kila mmoja atakaa kwa siti tena dirishani (window seat).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...