Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili imeanza programu ya kutoa huduma kwa njia ya mkoba ili kujenga uwezo wa Hospitali za Rufaa za Mikoa nchini hasa katika maeneo yenye upungufu wa watalaam au maeneo yenye watalaam lakini wanahitaji kuongezewa ujuzi zaidi katika fani mbalimbali. 

Hayo yameswa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Huduma kwa Wateja katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Aminiel Aligaesha wakati anazungumzia huduma hiyo.

Amesema kuwa utoaji wa huduma hiyo ni sehemu ya mpango mkakati wa Hospitali iliojiwekea kuhakikisha inatembelea Hospitali za Rufaa za Mikoa nchini ili kushirikiana nao katika kutoa huduma kwa wananchi ambao wangepewa rufaa kwenda Muhimbili kupata matibabu wakati huohuo ikijenga uwezo wa watalaam."Hospitali ya Taifa Muhimbili ina majukumu makuu matatu ambayo ni kutoa huduma za ubingwa wa juu, kufundisha na kufanya utafiti hivyo huduma kwa njia ya mkoba ni kiungo kikubwa cha jukumu letu hapa nchini," amesema Aligaesha. 

Ameongeza katika kutekekeleza majukumu hayo walifanya mawasiliano na hospitali kadhaa nchini na wenzao Hospitali ya Rufaa ya Musoma wamekuwa wa kwanza kuitikia mwito na kuwaomba wawatembelee."Hivyo tumepeleka timu ya watalaam 14 ili kutoa huduma kwa pamoja na kuwajengea uwezo katika maeneo ya upasuaji wa watoto na watu wazima, kina mama, njia ya mkojo, huduma za macho, huduma za upasuaji wa pua, koo na masikio." Aidha tumepeleka pia watalaam wa tiba ya dawa za usingizi na mtalaam wa patholojia katika timu hiyo. Timu hiyo itatoa huduma kwa muda wa siku tano mfululizo,"amesema.

Pia amesema wananatoa mwito kwa wananchi walioko Mkoa wa Mara na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma hizo zitakazotolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Musoma.

" Utaratibu wa kupata huduma ni uleule unaotumika katika Hospitali husika,"amesisitiza.Ameongeza wanatoa mwito kwa wananchi na wadau kujitokeza kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kutoa huduma mikoani hususani katika kuchangia huduma za usafiri, gharama za vifaa vinavyotumika kutoa huduma husika na matumizi mengine ili kufanikisha azma yao ya kuwafikia wananchi wengi zaidi na hatimaye kupunguza rufaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...