Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunamshikilia mtu mmoja aitwaye Bilenjo Paul, miaka 46, mkazi wa Igombe, kwa kosa la kupatikana na pombe ya moshi (gongo) kiasi cha lita arobaini (40) pamoja na dawa ya kulevya aina ya bhangi kiasi cha kilogram mbili (2) , huko maeneo ya Igombe Wilaya ya Ilemela Jiji na Mkoa wa Mwanza, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Tukio hilo limetokea tarehe 17.10.2018 majira ya saa 11:00hrs baada ya Polisi kufanya doria maeneo tajwa hapo juu na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na kiasi hicho cha pombe ya moshi/ gongo pamoja na dawa ya kulevya aina ya bhangi. Jeshi la Polisi tunaendelea na uchunguzi pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani. 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunatoa onyo kali kwa wananchi wote wanaojihusisha na shughuli hizo za uuzaji na utumiaji wa pombe haramu ya gongo na dawa za kulevya waache mara moja na endapo mtu/watu watabainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Katika tukio la pili, mwanafunzi mmoja wa shule ya secondary ya Sengerema high school aitwaye Ayoub Yahya @ Petro , miaka 19, anayesoma kidato cha 5 mchepuo wa PCB, mwenyeji wa Kyerwa-Kagera, amekutwa akiwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya neti (chandarua) aliokua ameifunga kwenye mti uliopo pembeni ya uwanja wa mpira wa shule hiyo, iliyopo Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.

Tukio hilo limetokea tarehe 18.10.2018 majira ya saa 06:00hrs asubuhi, hii ni baada ya wanafunzi wenzake kupita eneo la uwanja wa shule kisha kuona mwili wa marehemu ukiwa unaning’inia juu ya mti na kutoa taarifa kwenye uongozi wa shule ambao ulifikisha taarifa hizo kituo cha polisi.

Polisi tulifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kuukuta mwili wa marehemu mahali hapo. Chanzo cha mauaji hayo bado hakijafaamika, Polisi bado tunaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya DDH Sengerema kwa ajili ya uchunguzi pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwaajili ya mazishi. 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linatoa wito kwa wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili waweze kukamatwa na na kufikishwa katika vyombo vya sheria. 

Imetolewa na;
Advera Bulimba –ACP
Kaimu Kamanda wa Polisi (M) Mwanza
18, October 2018.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...