Na Mwandishi wetu, Kondoa

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa mkoani Dodoma, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu, maji, afya, miundombinu ya barabara na huduma nyingine za kijamii zimeimarika zaidi katika Jimbo la Kondoa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Dkt. Kijaji ameeleza hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika Jimbo lake katika Mkutano Mkuu Maalumu wa Jimbo la Kondoa uliowashirikisha zaidi ya wajumbe 1,200, uliofanyika katika Kata ya Pahi, wilayani Kondoa.

Ameyataja baadhi ya mafanikio makubwa kuwa ni kuchimba na kukarabati visima virefu na vifupi vya maji vipatavyo 56 pamoja na kukarabati visima vingine 4 vilivyoharibika zaidi ya miaka 15 iliyopita ambapo zaidi ya sh. bilioni 1.8 zimetumika, hatua iliyochangia wananchi zaidi ya laki moja katika Jimbo la Kondoa kuanza kupata huduma ya uhakika ya maji.

Kuhusu Sekta ya Elimu, Dkt. Kijaji ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa shule mbili mpya za Sekondari katika Kata za Hondomairo na Bumbuta kwa gharama ya sh. milioni 140.5, ambazo zitaanza kuchukua wanafunzi kuanzia mwezi Januari, 2019 pamoja na kujenga na kukarabati vyumba ya madarasa, mabweni na nyumba za walimu, kwenye shule mbalimbali za Sekondari na msingi.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa (CCM), Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi-CCM, katika kipindi cha miaka 3, katika Jimbo la Kondoa, wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Jimbo la Kondoa uliofanyika katika Kata ya Pahi, Kondoa, mkoani Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Mkoa wa Dodoma, Comrade Godwin Mkanwa, akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa, baada ya kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano katika Jimbo hilo, iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa (CCM), Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.

Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Amina Mollel, akifuatilia kwa makini matukio ya uwasilishwaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Kipindi cha Miaka 3 ya Serikali ya Awamu ya Tano katika Jimbo la Kondoa. Walioketi karibu naye ni wazazi wa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Mzee Abdallah Kijaji na mkewe Aziza Selemani, katika Kata ya Pahi, Kondoa, Dodoma

Sehemu ya umati wa wajumbe 1,200 wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Jimbo la Kondoa, wakipokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Kipindi cha Miaka 3 ya Serikali ya Awamu ya Tano katika Jimbo la Kondoa, iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, katika Kata ya Pahi, Kondoa, mkoani Dodoma.



KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...