Khadija Seif,Globu ya jamii
KAMPUNI ya Oval Technical Limited wametambulisha  application mpya ya kibiashara inayojulikana kama SMART MAUZO kwa lengo la kukabiliana na changamoto za kibiashara.

Meneja Mauzo wa kampuni hiyo Hamza Mohamed amesema leo jijini Dar es Salaam amesema  lengo la kuanzishwa kwa mfumo huo kuwa kumekuepo kwa changamoto nyingi nchini zinazowakabili wafanyabiashara.

Ametaja baadhi ya changamoto kama kutohifadhi taarifa sahihi za mauzo ya bidhaa zao na kupelekea kupata hasara katika biashara zao.

Pia amesema changamoto nyingine ni kutokua na uaminifu baina ya mmiliki na msimamizi kutofahamu idadi ya manunuzi yanayofanyika kila siku,wiki,mwezi Kwenye duka .

Mohammed amesema mfumo  huo utawawezesha wafanyabiashara wengi nchini kutatua changamoto zao na mpaka sasa zaidi ya wanafanyabiashara 200 wamejisajiri na huduma hiyo ya Smart Mauzo.

Aidha amesema , kujiunga na mfumo huo unaingia kwenye uwanja wa kupakua huduma za kimtandao na kuandika www.smartMauzo.com na kisha kulipia huduma hiyo kwa kiasi cha Sh.5000 za kitanzania na kwa mwezi na ukishasajiriwa utaweza kulipia Sh.3000 kwa kila mwezi.

Ametoa rai kwa ambao hawajajisajiri waweze kujisajiri ili kuleta chachu katika sekta ya biashara kwani kuna msemo usemao mali bila daftari huisha bila habari, hivyo basi daftari hilo ni mtandao huo ambao utawezesha kuandika kila taarifa ya manunuzi pamoja na bidhaa zilizodukani.
Meneja masoko kampuni ya oval technique limited Hamza Mohammed akizungumza na wanahabari wakati akitambulisha huduma ya smart Mauzo jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...