NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mwl. Raymond Mwangwala amewasihi wananchi wa jimbo la Jang’ombe hasa vijana kumchagua kwa kura za ndio mgombea wa tiketi ya CCM Ramadhan Hamza Chande. 
 Wito huo ameutoa leo alipokuwa akimnadi na mgombea wa CCM Jimbo la Jang’ombe huko katika Mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika Tawi la Kidongo Chekundu Unguja. Amemtaja mgombea huyo wa CCM kuwa ni mgombea pekee mwenye sifa na vigezo vya kuleta mabadiliko chanya ya maendeleo katika Jimbo hilo. 
 Mwl. Raymond amesema viongozi mbali mbali wa CCM katika Jimbo la Jang’ombe wametekelea kwa ufanisi miradi ya maendeleo na kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto sugu za jimbo. Pia ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya saba inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ametekeleza kwa ufanisi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2016 hatua ambazo zinastahiki kuungwa mkono na wananchi wote hasa wa Jimbo hilo. 
 Katibu Mkuu huyo wa UVCCM Raymond, amebainisha kwamba mafanikio hayo yatakuwa endelevu endapo wanachama na wananchi wa Jang’ombe watamchagua mgombea anayetokana na Chama Cha Mapinduzi chenye sera imara na historia ya kuwatumikia wananchi wa rika zote hasa vijana. 
 Katika maelezo yake Katibu Mkuu huyo alisema kupitia Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 2018/2019 zimetengwa jumla ya shilingi bilioni tatu kwa ajili ya kusaidia kundi la Vijana hatua ambayo inatakiwa kuthaminiwa na kundi hilo. 
 Alisema mbali na fedha hizo pia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayotokana na CCM inajenga viwanja vya kisasa vya michezo kwa kila Wilaya Zanzibar kwa lengo la kuwawezesha vijana wajiajiri kupitia sekta ya michezo mbali mbali. 
 Aidha alisisitiza kuwa CCM ina matarajio makubwa ya kushinda kwa asilimia kubwa katika uchaguzi huo kutokana na Wananchi hasa kuiamini na kuiunga mkono tasisi hiyo kwani ushahidi wa tathimini hizo umeonekana wazi katika Chaguzi za Majimbo mbali mbali ya Tanzania bara ambayo chama hicho kimeshinda kwa kishindo. 
 “Mgombea wetu anauzika ana mvuto na pia ana sifa ya utendaji na uchapakazi uliotuka hivyo nakuombeni wananchi wa Jimbo la Jang’ombe hasa Vijana Wenzangu Octoba 27, mwaka huu tumchague ndugu Ramadhan Hamza kwa kura nyingi za ndio”, alisema Mwl. Raymond. 
 Aliongeza kuwa Vyama vya upiunzani kwa sasa havina sera na vimepoteza dira ya kisiasa kwa kutawaliwa na migogoro na visasi vya wenyewe kwa wenyewe hali inayovikosesha sifa ya kuongoza nafasi yoyote katika jamii.
 WANACHAMA wa CCM na wananchi kwa ujumla walioudhuria katika mkutano wa kampeni za CCM wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi
 KATIBU Mkuu wa UVCCM Mwl.Raymond Mwangwala akiwahutubia wananchi katika kampeni za kumnadi mgombea wa CCM nafasi ya Uwakilishi Ramadhan Hamza Chande  katika Mkutano uliofanyika uwanja wa Tawi la CCM Kidongo Chekundu.
Mgombea uwakilishi tiketi ya CCM Jimbo la Jang’ombe  ndugu Ramadhan Hamza Chande(kushoto) akiomba kura za ndio katika mkutano huo ambao mgeni rasmi ni Katibu Mkuu wa UVCCM Mwl.Raymond Mwangwala(kulia) huko uwanja wa Kidongo chekundu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...