Na Mwamvua  Mwinyi, Bagamoyo
MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo, mkoani Pwani, Dk.Shukuru Kawambwa, amewatoa hofu wananchi watakaopaswa kupisha ujenzi wa barabara ya njia nne kuanzia Makofia -Mlandizi kwa kiwango cha lami kuwa watalipwa fidia utekelezaji utakapoanza. 

Aidha amewaeleza, wakala wa barabara (TANROADS) bado haijawa tayari katika utekelezaji huo lakini wale wanaopitiwa na bomba kuu linaloelekea Bagamoyo ,kuanzia eneo la Sunguvuni -Sanzale watarajie kulipwa fidia zao na DAWASA hivi karibuni . 

Akitolea ufafanuzi suala hilo kwa wakazi wa Chasimba na Magoza,kata ya Yombo wakati wa ziara yake ya kata kwa kata, Kawambwa alisema walengwa wanaoguswa na miradi hiyo wavute subira. 

Aidha alieleza, ahadi ya malipo ambayo DAWASA  italipa anaendelea kufuatilia ili kupata taarifa zaidi ya malipo hayo . 

"Serikali imedhamiria kuboresha miundombinu ya barabara mbalimbali, hii barabara nayo ipo katika utekelezaji wa ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi, "

"Tanroads na DAWASA wamekubaliana wakati ikisubiriwa kufikia ujenzi wa  barabara hiyo, imeingiliana na mradi wa bomba kuu la maji ambapo DAWASA italipa wale  watakaopitiwa na ujenzi huo "alifafanua Kawambwa. 

Kuhusu barabara ya Yombo-Kiegea ,mbunge huyo alisema inatafutwa fedha ili iweze kuboreshwa kwa kiwango cha changalawe .

"Kwa bajeti ya mwaka 2018/2019 TARURA haina fedha hivyo kwasasa ni matengenezo madogo madogo wakisubiri utengenezaji mkubwa baadae endapo kukipatikana fedha"alibainisha .

Akijibu suala la ukosefu wa umeme huko Chasimba na Magoza alisema maeneo hayo yameingizwa katika mradi wa Peri Urban na mkandarasi atakapopatikana watarajie kunufaika na mradi huo mpya. 

Awali wakazi wa Chasimba, Magoza kata ya Yombo walisikitishwa umeme kuwekwa mijini na vijiji kusahaulika kwa miaka mingi. 

Walisema ,wanatumia solar kila siku kwa gharama ya sh.3,000, gharama ambayo ni kubwa kwao kwa maisha ya sasa .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...