Na Shushu Joel,Chalinze
VIJANA wengi nchini wamejikuta wakikumbana na changamoto nyingi katika utafutaji wa maisha katika jamii zao na kupelekea kundi jingine kujiunga katika matumizi hatari ya utumiaji wa madawa ya kulevya na hivyo hata taifa kukosa vijana wa kuitumikia serikali yao.


Kukithili kwa vitendo vya uvutaji wa bangi vijiweni kunasababishwa na wazazi walio wengi kwa kutojenga tabia ya kuwakanya watoto wao pindi wanapokuwa wadogo na hata inapotokea watoto wao kupewa hadhabu ya viboko na walimu au watu wengine wazazi wamekuwa wakiwaijua juu wale waliojitokeza kuwakanya watoto hao.

Akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Chalinze katika mahafari ya shule hiyo mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete amewataka vijana kutokaa vijiweni na watu walioshindikana kwani watawashawishi vibaya na hata kuwataka waweze kujiunga katika makundi ambayo si mazuri.

Alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wakishawishiwa na watu wenye nia mbaya na vijana ili kuwaona tu na wao wanaharibika kwa kufuata matendo mabaya wanayoyafanya kwenye mitaa ikiwemo ubakaji,uvutaji wa madawa ya kulevya na hata kwenye wizi.

Kikwete aliongeza kuwa serikali inawategemea kwa kiasi kikubwa ili muweze kuja kuisaidia katika Nyanja mbalimbali pindi mtakapokuwa wakubwa kwani uongozi ni mchezo wa kupokezana.

“Mimi mbunge wenu nawahakikishieni serikali ya awamu ya tano imekuwa imejiwekea mikakati mikubwa ya kuhakikisha vijana wote wanamaliza masomo yao na wanafaulu ni lazima waende shule bila cha kusingizia kukosekana kwa ada,hivyo nawatakeni wanafunzi wote katika jimbo la chalinze kuhakikisha kila mmoja wenu anafaulu ili kuja baadae kuisaidia serikali na Taifa kwa ujumla.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Chalinze katika mahafari ya shule hiyo.




Baadhi ya wananfunzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...