NAODHA wa timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu chini ya Miaka 18 Jesca Ngisaise anatarajia kusafiri kesho alfajiri  kuelekea Senegal kwenye majaribio.

Jesca amekuwa zao zuri la vijana katika mchezo wa kikapu nchini akionekana kufanya vizuri pale anapokuwa anapewa nafasi na kama atafanikiwa kufanya vizuri kwenye majaribio hayo atapata nafasi ya kujiunga na NBA ACADEMY. 

 Kama Jesca atafanikwia kujiunga na NBA Academy atakuwa amepiga hatua moja kubwa sana kuelekea kucheza kwenye WNBA nchini Marekani. 

Jescar mwenye umri wa  miaka 17 na amekua akifanya vizuri katika timu ya Taifa pia aliweza kuchagulia katika timu ya All Stars kwenye mafunzo maalumu ya BWB yaliyofanyika kule Africa kusini mwezi wa nane. Tunamtakia kila la heri aendelee kutuwakilisha vyema. 


Hapa nyumbani Jescar anacheza katika timu ya Ukonga Academy na katika ligi ya mkoa wa Dar es salaam iliyomalizika hivi karibuni alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi hiyo.
Naodha wa timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu chini ya Miaka 18 Jesca Ngisaise.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...