*Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo Dk. Mwandolela azungumzia mfumo wa maisha unavyochangia

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KLINIKI ya Magonjwa ya Moyo Heameda iliyopo Bunju B jijini Dar es Salaam imeanzisha kambi maalumu ya siku mbili kwa lengo la kupima na kufanya uchunguzi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza yakiwemo ya moyo huku ikielezwa sababu za kuongeza kwa magonjwa hayo ni mfumo wa maisha.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa kambi hiyo Mkurugenzi wa Kliniki hiyo ambaye pia ni Daktarii Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Dk. Hery Mwandolela amesema watatoa huduma hiyo kwa siku tatu kuanzia leo, kesho na keshokutwa watafunga rasmi ambako mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Reginald Mengi.

Amesema kuwa wameamua kutenga siku hizo kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kwa wananchi mbaliimbai ambao wamefika kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza na kwamba uamuzi huo ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii ya Watanzania.

“Tunatoa mwito kwa wananchi waje wapime afya zao bure, Heameda tumeamua kutoa huduma ya matibabu kama sehemu ya kutoa shukrani kwa wananchi wote.Hivyo kwa mwaka huwa tunatenga siku maalumu za kuwa na kambi hiyo.Kwa leo waliofika hadi saa saba mchana ni watu zaidi ya 130 na wanaendelea kuja.Nasi tunawakaribisha maana tupo kwa ajili ya kuwahudumia,”amesema Dk.Mwandolela.

Kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza nchini amesema kasi imekuwa kubwa sana na takribani kwa miaka 30 hali inazidi kuwa mbaya hasa katika magonjwa ya kupanda kwa shinikizo la damu, sukari na saratani.”Mfumo wa vyakula tunavyokula na kutofanya mazoezi ni moja ya sababu kubwa ya magonjwa hayo.Pia msongo wa mawazo nao umechangia kuongeza kwa ugonjwa wa kupanda kwa shinikizo la damu,”amefafanua.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo . Dk. Henry Mwandolela wa Heameda Madical Clinic akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali yake iliyoko Bunju B jijini Dar es salaam wakati wa kambi ya siku mbili ya uchunguzi wa Magonjwa mbalimbali inayofanyika hospitalini hapo kuanzia saa mbili asubuhi mpaka jioni , Kiliniki hiyo itafungwa rasmi ziku ya jumamosi 
Baadhi ya madaktari wakiendelea kutoa huduma kwa wananchi mbalimbali waliokwenda kupata huduma ya matibabu 
Baadhi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo wakitoa huduma kwa wananchi waliofika katika kambi hiyo.
  
Baadhi ya wananchi wakisuburi huduma wakati kambi hiyo ikiendelea kwenye hospitali ya Heameda Medical Clinic.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...