Na Mwandishi Maalumu, Riyadh- Saudi Arabia 
 Kundi la madaktari bingwa 14 wa hiyari kutoka nchini Saudi Arabia linatarajiwa kuwasili Zanzibar tarehe 12 Oktoba ambapo wataweka kambi ya tiba (medical camp) kwa muda wa siku 10. Madaktari hao wanatarajiwa kufanya matibabu na upasuaji katika hospitali za kisiwa cha Pemba. 
 Akizungumza katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini Riyadh wakati wa hafla ya kuagana na madaktari hao, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza, alisema kambi tiba hii ni ya tatu kufanyika Zanzibar. 
Mwezi Novemba mwaka 2016 madaktari hao walifika Zanzibar na kuweka kambi ya kwanza katika kisiwa cha Pemba Iliyojulikana kama (Surgical Caravan 1) kwa mara ya kwanza kwa mafanikio makubwa. Mwezi Oktoba 2017 pia walifanya kambi ya pili iliyojulikana (Surgical Caravan 2) katika hospitali za kisiwa cha Pemba. 
 Katika safari yao miaka miwili iliyopita madaktari hao walipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wa Wizara ya Afya ya Zanzibar na madaktari wenyeji, ndio maana wamependelea kurejea tena mwaka huu kufanya kambi ya tatu (Surgical Caravan 3). 
 Pamoja na kutoa huduma za matibabu, madaktari hao watasafiri na dawa na vifaa tiba vya aina mbalimbali ambavyo Mwisho wa kambi watavitoa kama msaada kwenye hospitali hizo.
Viongozi wa Madaktari wa Saudi Arabia wakiwa na Balozi Hemedi Mgaza walipofika Ubalozi mjini Riyadh kuaga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...