Na Aisha Abdallah, Mahakama Kuu Tabora

Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Mhe. Salvatory Bongole amefungua rasmi Mafunzo ya Mahakimu na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata mkoani humo yanayolenga kuwajengea uwezo wa kuyasimamia mabaraza ya kata katika utekelezaji wa majukumu kwa mujibu wa sheria.

Akifungua Mafunzo hayo mapema Oktoba 08, katika Ukumbi wa Katibu Tawala, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Bongole aliwaelezea washiriki wa mafunzo hayo kuwa ni muhimu kwa sababu yataleta uelewa wa pamoja kati ya Mahakama na Mabaraza ya Kata juu ya mamlaka ya Mahakama na Mabaraza katika utoaji haki.

Aidha katika hotuba yake ya ufunguzi,Mhe. Jaji Mfawidhi huyo pia alisisitiza kuhusu umuhimu wa kumsikiliza mtu kabla ya kutoa maamuzi na kuwaasa wanasemina kuyatekeleza mambo yote watakayojifunza katika semina hiyo. “Kama sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama suala la ushirikishwaji wa Wadau limepewa kipaumbele ili tuweze kufanikisha huduma ya utoaji haki”, alisema Mhe. Jaji Bongole.

Katika semina hiyo, Mahakama imewashirikisha Wanasheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora na Halmashauri ya Manispaa-Tabora kama viongozi wa Mabaraza ya Kata. Mafunzo hayo ya siku tatu yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania na kuendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).

Washiriki ni Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo kutoka Tabora Mjini, Urambo, Nzega na Igunga pamoja na wajumbe wa Mabaraza ya
Kata na Wanasheria wa Halmashauri ya Manispaa na wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora


Sehemu ya Washiriki wakiwa katika Mafunzo hayo. 
Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Mhe. Salvatory Bongole (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata wanaoshiriki katika Mafunzo ya siku tatu, Oktoba 08, 2018 hadi Oktoba, 10, 2018. 
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Mhe. Salvatory Bongole  (katikati) ambaye pia alikuwa Mhe. Mgeni rasmi wa Mafunzo hayo, akiwa katika picha ya pamoja na Wanasheria wa Manispaa ya Tabora (waliosimama). 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...