Na.WAMJW,Mbeya

Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yameleta mahangaiko pamoja na athari kwa jamii wa Mkoa wa mbeya ikiwepo ulemavu

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa MbeyaSerikali Mkoani Mbeya imesema kuwa nchi zilizo katika Ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo zinakabiliwa na tatizo la magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele zimeathiri sehemu kubwa ya jamii Mkoani hapa na kuleta mahangaiko kwa wananchi pamoja na ulemavu.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila wakati wa ufunguzi wa semina ya uraghibishaji na uhamasishaji wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa viongozi wa Serikali wa Mkoa na wilaya mkoani hapa.Alisema Magonjwa hayo yamekuwa yakiathiri zaidi wananchi na kiasi kikubwa yakipunguza uwezo wa wananchi katika shughuli za uzalishaji na ujenzi wa Taifa.

“Magonjwa haya, pamoja na kusababisha usumbufu mkubwa kwa waathirika pia yanaongeza matumizi ya rasilimali chache tulizonazo katika kuyakabili “alisema Mkuu huyo mkoa.Aidha,Chalamila alisema kwamba uwepo wa magonjwa hayo umefanya watoto kutokuwa na mahudhurio mazuri mashuleni kutokana na muda mwingi kuwa wanaumwa.Hata hivyo alisema kuwa jambo la kutia moyo ni kwamba Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau wamekuwa wakitoa Kingatiba za kukinga magonjwa haya katika mkoa wa Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akifungua semina ya uraghibishaji na uhamasishaji wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa viongozi wa mkoa na Wilaya kwenye ukumbi wa halmashauri wa Benjamin Mkapa Jijini Mbeya.Kulia ni Ofisa mpango toka Wizara ya Afya Osca Kaitaba na mwisho ni Mkuu wa Wilaya ya Kyela Bi.Claudia Kitta.
Ofisa Mpango toka Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Osca Kaitaba akifafanua jambo kwenye mkutano huo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...