Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Dkt. Nyabisi Malyatabu ambaye ni Meneja wa Kanda wa Taasisi ya Utafitiwa Kahawa Tanzania (TACRI), Maruku mkoani Kagera  kuhusu kilimo bora cha kahawa wakati  alipotembelea  Taasisi hiyo, Oktoba 9, 2018. Watatu kushoto ni Naibu Waziri wa kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mhogo aina ya tegemeo unaostawi vizuri katika maeneo ya Kanda ya Ziwa  wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti cha Maruku mkoani Kagera, Oktoba 9, 2018. Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt, Mary Mwanjelwa na kushoto ni Mkuu wa Kituo, Innocent Ngyetabwa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vyakula mbalimbali vilivyotengenezwa kwa kutumia unga wa mhogo, ndizi na nafanka nyingine wakati alipotembelea kituo cha Utafiti  cha Maruku mkoani Kagera, Oktoba 9, 2018. Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt, Mary Mwanjelwa na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Chuo cha  Kilimo - MATI- Maruku, Laurent Luhembe. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama uzalishaji wa miche ya Kahawa bora kwa kutumia majani ya kahawa wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI)  cha Maruku mkoani Kagera, Oktoba 9, 2018.  Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera,  Brigedia Jenerali, Marco Elisha Gaguti na wapili kushoto ni Afisa Ugani wa TACRI, Aretas Urassa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...