Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali zote mbili, yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dkt. Ali Mohamed Shein zinaamini kuwa vyama vya Ushirika ni njia muhimu sana ya kuzalisha ajira hususan kwa wanawake na vijana.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos uliofanyika katika ukumbi wa Abdul Wakiil, Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni, Zanzibar.Ushirika wa Mamlaka Saccos ulianza na wanachama 55 na mpaka sasa wakati wa uzinduzi wake una wanachama 250 pamoja na mambo mengine Ushirika huo umeshatoa mikopo bila riba shilingi milioni 93 kwa wanachama 133.

Makamu wa Rais aliwapongeza wanaushirika huo kwa kusema “Ni wazo zuri sana kama mtalisimamia na kulitekeleza ipasavyo kwa haika mtajikomboa kiuchumi na kubadilisha kwa kiasi kikubwa hali zenu za maisha”Makamu wa Rais aliendelea kusema kuwa Binafsi anaamini sana katika ushirika tena ushirika wa kuweka na kukopa kwani ni moja ya njia sahihi ya kujikomboa kiuchumi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewaomba wananchi wa Zanzibar kupinga kwa nguvu zote masuala ya udhalilishaji na ukatili kwa wanawake na watoto na kuwataka watoe ushirikiano na Serikali katika mapambano dhidi ya udhalilishaji pia aliwahimiza wananchi hao kutunza mazingira kwa faida ya sasa nay a baadae.

Wakati huohuo Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Mhe. Moudline Castico amewataka wanachama wa Saccos hiyo kufanya kazi kwa bidii na si kwa mazoea.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa ameshikilia bango lenye maneno ya uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos kama ishara ya uzinduzi rasmi, kushoto ni Mwenyekiti wa Ushirika Ndugu Mohammed Khamis Ali. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha picha yake aliopewa kama zawadi wakati uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos kama ishara ya uzinduzi rasmi, wengine pichani ni Waziri wa Kazi Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Mhe. Moudline Castico (kulia) kushoto ni Mwenyekiti wa Ushirika Ndugu Mohammed Khamis Ali. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos kwenye ukumbi wa Abdul Wakiil, Baraza la Wawakilishi la Zamani, Kikwajuni, Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos kwenye ukumbi wa Abdul Wakiil, Baraza la Wawakilishi la Zamani, Kikwajuni, Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...