BENKI ya NMB imetoa mafunzo ya kibenki kwa mawakala wake kutoka Kanda saba nchini ili kuboresha huduma kwa wateja na kukuza biashara zao. Mafunzo hayo yaliotolewa kwa mawakala wa NMB, ambao wanasaidia kutoa huduma za kibenki kwa wateja, yametolewa kwenye Kanda 7, ambazo ni pamoja Nachingwea, Newala, Tandahimba, Mbeya, Dodoma, Morogoro, Arusha, Tabora na Mwanza.

Benki ya NMB iliamua kuwajengea uwezo mawakala wake ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja pindi wanapowahudumia. Katika mafunzo hayo, mawakala walipata elimu kutoka kwa wataalam wa masuala ya kibenki pamoja na timu ya mtandao wa kanda husika. Miongoni mwa mafunzo hayo ni pamoja na uelewa juu ya huduma na bidhaa mbalimbali za benki,

Pamoja na hayo, NMB ilitoa motisha na kutambua michango ya mawakala waliofanya vizuri katika kutoa huduma hizo. Baadhi walipata zawadi mbalimbali na vyeti maalum kwa wakala aliyefanya vizuri kwa kila Kanda. Ujuzi huo utaendelea kutolewa kwa maeneo yaliosalia. Benki ya NMB kwa sasa ina zaidi ya mawakala 6000 nchi nzima.
Meneja wa NMB kanda ya ziwa - Abraham Augustino, akizungumza na mawakala wa benki hiyo kwenye kongamano la mawakala lililofanyika Jijini Mwanza jana. NMB inaendesha semina ya mawakala zaidi ya 6,000 ili kuwajengea uwezo na kutambua mchango wao katika kutoa huduma za kibenki nchini. 
Mmoja wa wakala akitunukiwa cheti baada ya kufanya vizuri katika biashara yake. 
NMB inaendesha semina ya mawakala zaidi ya 6,000 ili kuwajengea uwezo na kutambua mchango wao katika kutoa huduma za kibenki nchini. Baadhi ya mawakala wakiwa katika kongamano la mafunzo. 
Wakala wa NMB kutoka wilayani Chato Mkoani Geita - Suleiman Rweikondo, akionesha cheti cha mshindi wa wakala bora namba moja kwa kanda ya ziwa wakati wa kongamano la mawakala liliofanyika jijini Mwanza jana.NMB inaendesha semina ya mawakala zaidi ya 6,000 ili kutambua mchango wao katika kutoa huduma za kibenki nchini. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...