Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) amekabidhi msaada wa Vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 36.5 kwa ajili ya vituo vya afya na zahanati sita zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Msalala na Kahama Mji wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Mheshimiwa Azza amekabidhi vifaa tiba hivyo leo Jumanne Oktoba 16,2018 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Anamringi Macha wakati wa Kikao cha Baraza la UWT wilaya ya Kahama uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kahama.
Vifaa tiba hivyo ni pamoja na shuka 100,mashine za kupima damu,wingi wa damu,sukari,joto,mapigo ya moyo na vifaa vya kusaidia kujifungua kwa akina mama ambavyo kupatikana kwake kumetokana na jitihada za mbunge huyo kuhakikisha vifo vya mama na mtoto vinapungua mkoani Shinyanga.
Awali akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa tiba hivyo,Mheshimiwa Azza Hilal alisema kupitia Kampeni yake ya ‘Afya Yangu Mtaji Wangu’ na kuwajali akina mama aliamua kutafuta wadau kwa ajili ya kusaidia kumaliza changamoto ya uhaba wa vifaa tiba katika vituo vya afya na zahanati.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati akikabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 36.5 kwa ajili ya zanahati na vituo vya afya wilayani Kahama leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kahama.Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kahama,Telephora Saria,kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga. 
Vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 36.5 kwa ajili ya zanahati na vituo vya afya wilayani Kahama vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) kwa kushirikiana na wadau wake Bahari Pharmacy Ltd na Brett &Beileys.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi vifaa tiba kwa  Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi shuka ikiwa ni sehemu ya shuka 100 alizotoa kwa ajili ya vituo vya afya na zahanati wilayani Kahama.
Wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akiwa ameshikilia boksi lenye mashine ya kupimia sukari mwilini. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga.Wa kwanza kushoto ni  Mbunge wa Jimbo la Ushetu,Mheshimiwa Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akifuatiwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa ameshikiliwa vifaa tiba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...