NA MWANDISHI WETU:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) amepongeza kazi za uzalishaji mali katika kambi ya Mlale.

Aliyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi kwenye kambi hiyo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) iliyopo Mlale kwa lengo la kuzungumza na kuangalia miradi mbalimbali ya uzalishaji mali kambini hapo.

Waziri Mhagama alisema kuwa dira ya taifa kufikia 2025 ni kuongeza harakati za maendeleo ya uchumi na jamii kufikia hadhi ya uchumi wa pato la kati kwa kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati hapa nchini inayolenga kuleta maendeleo ya wananchi na Taifa.  

“Miradi hii iliyoanzishwa hapa imekuwa na tija kubwa kwa jamii iliyokaribu katika kufanikisha upatikanaji wa ajira kwa vijana na kukuza uchumi na maendeleo ya wanamlale na watanzania kwa ujumla” alisema Mhe. Mhagama

Aliongeza kuwa, mageuzi ya kikosi cha JKT Mlale 842 yamekuwa ni makubwa sana hususan katika kuunga mkono maagizo ya Mhe. Rais, Dkt. John Magufuli kwa kuanzisha kiwanda cha kuchakata sembe kwa uwezo mkubwa na kuzalisha tani 440 kwa mwezi.

Aidha, Mheshimiwa Mhagama alihamasisha kikosi hicho kuendelea kutoa mafunzo kwa vijana ikiwa ni njia moja wapo ya kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwezesha vijana kupata mafunzo ya stadi za kazi yatakayowawezesha kupata ujuzi wa kuweza kujiajiri na kuajiri.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na Kikosi 842 cha Jeshi Kujenga Taifa (JKT) Mlale, alipofanya ziara ya kikazi kuona shughuli za uzalishaji mali zinazofanywa na kikosi hiko.
 Mkuu wa Kikosi Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mlale, Luteni Kanali Al Solomon Shausi akielezea miradi ya  uzalishaji mali iliyopo kwenye kambi hiyo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi kuona shughuli za uzalishaji mali zinazofanywa na kikosi hiko.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa Mwendesha Mitambo ya Kiwanda SG. Vereranda Kihali jinsi shughuli ya uchakataji sembe inavyofanyika katika kiwanda hiko, alipotembelea kambi ya JKT Mlale 842 kujionea shughuli za uzalishaji mali katika kambi hiyo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimjulia hali mtoto Hawa Mapunda, aliyelazwa (kulia) ni mama wa mtoto Bi. Christer Ndomba alipotembelea wodi ya watoto katika kituo cha afya cha JKT Mlale, Peramiho, akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikabidhi mashuka kwa viongozi wa kambi ya JKT Mlale, alipofanya ziara kwenye kambi hiyo kujionea shughuli za uzalishaji mali.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...