Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kampeni jimbo la Jang`ombe ambapo Chama Cha Mapinduzi kimemsimamisha Bw. Ramadhan Hamza Chande kugombea nafasi ya Uwakilishi katika jimbo hilo.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa, Makamu wa Rais amewataka wakazi wa Jang`ombe kufuata nyayo walizoachiwa na Wazazi wao.Mheshimiwa Samia amewambia wakazi wa jimbo hilo kuwa atatoa ushirikiano wa kutosha kwa kufanya kazi pamoja na Viongozi wa Jimbo hilo katika kuboresha huduma za afya na elimu.

Pamoja na Viongozi wengine Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mbunge mteule wa jimbo la Liwale kutoka mkoani Lindi Bw. Zuberi Kachauka ambaye aliwaambia wakazi wa Jimbo la Jang`ombe kuwa upinzani umekufa kwa kukosa sera na viongozi bora.

Kampeni za Uwakilishi jimbo la Jang`ombe zilianza tarehe 14 Oktoba na zinatazamiwa kukamilika tarehe 25 Oktoba 2018 na tarehe 27 Oktoba wananchi watapiga kura kumchagua Mwakilishi wa jimbo hilo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa mkutano wa kumnadi mgombea wa Uwakilishi jimbo la Jang`ombe kwenye viwanja vya Baja.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na Katiba ya Chama mgombea wa CCM nafasi ya Uwakilishi Jimbo la Jang`ombe Bw. Ramadhan Hamza Chande wakati wa mkutano wa kumnadi mgombea wa Uwakilishi jimbo la Jang`ombe kwenye viwanja vya Baja. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Wahamasishaji wakiwa wamebeba picha ya mgombea wa nafasi ya uwakilishi kupitia CCM jimbo la Jang`ombe Bw. Ramadhan Hamza Chande wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Baja ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Dkt. Abdulla Juma Sadala wakati wa mkutano wa kumnadi mgombea wa Uwakilishi jimbo la Jang`ombe kwenye viwanja vya Baja.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo wakati wa mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa Uwakilishi jimbo la Jang`ombe kwenye viwanja vya Baja kushoto ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid.
Bendi ya Muziki wa Taarab ya Big Star ya CCM Zanzibar ikitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa CCM wa jimbo la Jang`ombe kwenye viwanja vya Baja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...