Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) Dkt. Anold Mathias Kihaule, ameenza kazi kwa kukagua utendaji wa ofisi za Usajili za Mkoa wa Dar-es-salaam ambapo pamoja na mambo mengine amezungumza na wananchi na kutembelea ofisi ya Serikali ya Mtaa ambako huduma ya utoaji wa fomu na ugawaji wa Vitambulisho zinaendelea.

Katika ziara hiyo Dkt. Kihaule aliyekuwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa Mamlaka hiyo; amepongeza kazi nzuri inayofanywa na wafanyakazi wa NIDA na kusisitiza watumishi kuzingatia utoaji wa huduma unaozingatia viwango ili kuweza kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima kwa wananchi.

Aidha amewashukuru viongozi na Watendaji katika Serikali za Mitaa kwa kazi nzuri ya kuwahudumia wananchi kuhakikisha wanapata Vitambulisho vya Taifa na kuahidi kuendelea kuwapa ushirikiano katika kuhakikisha malengo ya Serikali yanafikiwa.

Dkt. Anold Mathias Kihaule aliteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo akijaza nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Andrew W. Massawe aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Ajira na Walemavu.

Pichani ni mmoja wa wakazi wa Kinondoni akimuelezea Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulish vya Taifa(NIDA), Dkt. Anold Mathias Khaule (wa pili kushoto) namna alivyopatiwa huduma katika ofisi ya Usajili Wilaya ya Kinondoni
Mkurugenzi Mkuu wa NIDA akikagua fomu ya mmoja wa wananchi waliojitokeza kusajiliwa. Kutoka kulia ni Bw Dickson Mbanga Afisa Usajili wilaya ya Kinondoni na katikati ni Bw. Alphonce Malibiche, Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa.
Mkurugenzi Mkuu NIDA akikagua sehemu ya kutunzia Vitambulisho vya Taifa katika ofisi ya Usajili wilaya ya Kinondoni. Kuli ni Afisa Usajili wilaya ya Kinondoni na wa kwanza kushoto ni Bw. Melkiory Ndofi Mkurugenzi wa Idara ya Fedha na Utawala.
Mkazi wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Gift Emmanuel Nkya (aliyevaa nguo nyeusi) mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo cha Biashara CBE, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa NIDA alipotembelea kituo cha Usajili Kawe jijini Dar-es-salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Dkt. Anold Mathias Kihaule akiweka saini katika kitabu cha wageni ofisi ya Usajili wilaya ya Kinondoni wakati alipofanya ziara kukagua namna shughuli za Usajili zinavyofanyika kituoni hapo
Mkurugenzi Mkuu wa NIDA (aliyevaa koti) akiingia kwenye ofisi ya Serikali Mtaa wa Mzimuni wakati wa ziara yake kukagua uendeshaji shughuli za Usajili Wilaya ya Kinondoni. Hapa alishuhudia utaratibu wa ugawaji fomu za Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi na utaratibu wa kugawa Vitambulisho vya Taifa kupitia ofisi za Watendaji.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...