Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
WANANCHI
wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wameelezwa kuwa wana kila sababu za
kuhakikisha wanakuwa na afya bora na salama, kwani afya ni muhimu na afya
ni mtaji mkubwa katika maisha ya binadamu.
Pia
wamehimizwa kupima afya zao kwa lengo la kutambua iwapo wamepatwa na
maambukizi ya UKIMWI au laa, kwani kwa atakaepatwa na ugonjwa huo
ataanza kutumia dawa ya ARV na hivyo ataishi maisha marefu.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo
wakati akizungumza na wananchi kuhusu kampeni inayoendelea ya
kupambana na UKIMWI na kujenga jamii yenye uelewa na furaha.Kizigo
amesema mbele ya wananchi kuwa Serikali ilianzisha kampeni ya Furaha
Yangu iliyozinduliwa kitaifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kwa Mkoa
wa Ruvuma ilizinduliwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto Ummy Mwalimu Agosti 31 mwaka huu 2018
"Wilaya
ya Namtumbo tumeendelea na kampeni hii ikiwa na lengo kuu la kuongeza
kiwango cha upimaji wa VVU hasa kwa wanaume na wananchi kwa ujumla. Hadi
juzi Oktoba 18 mwaka huu wa 2018 Wilaya ya Namtumbo walipima wanaume
873 na 16 walipatikana na VVU ambao kati yao 13 wameshaanza dozi
(ARVs)," amesema.
Ameongeza
kuwa Wilaya ya Namtumbo wameendeleza jitihada hizo kwa kuanzisha ligi
ya mpira wa miguu iitwayo Laigwanani Supwr Cup ambapo Laigwanani ni neno
la kimasai linalomaanisha Kijana na lengo ikiwa ni kuhamasisha vijana
kujitokeza kupima, kujitambua afya zao na watakaokutwa na VVU kuanza
dozi mapema.Mkuu huyo wa
Wilaya amewaambia wananchi hao kwa watakaobainika kuwa na virusi vya
UKIMWI dawa zipo na wataishi miaka mingi na kwamba anajua vijana
wanaogopa kupima kwa kuhofia njia ambazo wamezipitia.
Amewashauri
wananchi kujitokeza na kupima afya na watambue afya ni mtaji muhimu
katika maisha na ndio maana wilaya ya Namtumbo imeona umuhimu wa kampeni
hiyo ya kuhamasisha kupima UKIMWI ikaendelea na lengo ni kihakikisha
afya za wananchi zinakuwa salama.Pia
amewashauri kwa wale ambao hawapo ndani ya ndoa wawe waache kujihusisha
na ngono zembe na wasubiri hadi watakapoingia kwenye ndoa au wawe na
wakishindwa basi wawe na mpenzi mmoja na wawe wanatimia mpira ili
kujikinga na maambukizi.
Kizigo
ameongeza ni vema vijana wakatambua wao ni Taifa la leo na kesho na
hivyo kujilinda kwa kuwa na afya njema ni jambo la msingi kwani wakiwa
na afya njema watakuwa na fursa ya kujituma kwa ajili ya maendeleo yao
,wilaya,mkoa na taifa kwa ujumla.
Mkuu
wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo akisalimiana na mmoja wa Marefa
watakaokuwa wakichezesha Ligi hiyo ya mpira miguu iitwayo
LAIGWANANI SUPER CUP, Lengo ikiwa ni kuhamasisha
vijana kujitokeza kupima, kujitambua afya zao na watakaobainika kuwa na
maambuziki ya VVU wataanza dozi mapema.
Pichani
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo akisalimiana na baadhi
wachezaji wa timu walioshiriki ligi ya mpira wa miguu iitwayo
LAIGWANANI SUPER CUP, Lengo la kuanzishwa kwa Ligi hiyo ni kuhamasisha
vijana kujitokeza kupima, kujitambua afya zao na watakaobainika kuwa na
maambuziki ya VVU wataanza dozi mapema.
Mkuu
wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo akikabidhiwa taarifa kutoka kwa
Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo,kabla ya kuanza kwa mchezo wa Ligi ya mpira
wa Miguu iitwayo LAIGWANANI SUPER CUP.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...