Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
MTANGAZAJI maarufu nchini Isaac Muyenjwa Gamba ambaye alikuwa akitangaza Idhaa ya Kiswahiliya DW ya Ujerumani amefariki dunia leo akiwa nyumbani kwake mjini Bonn nchini 
Ujerumani.

Taarifa ambazo Michuzi Blog imezipata kutoka kwa wafanyakazi wa DW ambao walikuwa wakifanya naye kazi kabla kifo kumkuta wanasema kwa sasa wanaendelea kufanya mawasiliano na familia yake ili kupata maelekezo.

Wamesema kifo cha Gamba kimewasikitisha na kimewashangaza kwani baada ya kuona hakufika ofisini juzi,jana na leo waliamua kutoa taarifa Polisi na walipoenda nyumbani kwake walivunja mlango na baada ya kuingia ndani walimkuta akiwa tayari amefariki dunia.

Wamesema baada ya Polisi wa nchini humo kuingia ndani waliukuta mwili wa Gamba kwenye kochi.Hivyo wakati wakifanya mawasiliano na familia pia wanasubiri uchunguzi wa Polisi kwanza na kisha waendelee na taratibu nyingine.

"Kwa upande wetu huku Ujeruman tunaendelea kuwasiliana na familia yake wakati tukiendelea kusubiri majibu ya taarifa za uchunguzi wa Polisi," amesema mmoja wa wafanyakazi wa DW aliyeomba jina lake lihifadhiwe kwa nia njema tu.

Gamba wakati wa uhai wake pia amewahi kutangaza Redio One na ITV na kabla ya hapo pia amewahi kutangaza Redio Uhuru na RFA ambapo aina ya utangazaji wake na sauti yake vilimfanya kuwa maarufu nchini Tanzania.

Mungu amlaze mahala pema peponi. Ameen
MTANGAZAJI maarufu nchini Isaac Muyenjwa Gambaa akiwa kazini enzi za uhai wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...