Marehemu Ahmed Jongo enzi za uhai wake alipohojiwa na Azam TV

 Maziko ya Mtangazaji wa RTD Ahmed Jongo  yamefanyika leo  makaburi ya Mbagala Charambee Dar es Salaam
 Mtangazaji mkongwe na mmiliki wa redio ya Sports FM Abdallah Idrissa Majura akijumuika na ndugu, Jamaa na marafiki kupata chakula nyumbani kwa marehemu Tandika Maghorofani leo mchana kwenye mazishi ya aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo
.

  Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa ambaye pia ni Rais Mstaafu wa TFF na mchezaji mkongwe wa Yanga na Taifa Stars Leodegar Chilla Tenga (sahiti la buluu) na aliyewahi kuwa kiongozi wa Yanga Emmanuel Mpangala wakiungana na ndugu, jamaa na marafiki kupa pata chakula cha mchana nyumbani kwa marehemu aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam.

  Waombolezaji wakijadiliana jambo katika msibani  wa marehemu aliyekuwa Mtangazaji nguli wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni aliyekuwa Meneja wa Uwanja wa Taifa Mzee Frank Macha, mtangazaji Mkongwe Salim Mbonde na mwanasoka guli wa zamani ambaye sasa ni kocha Abdallah King Kibaden.
.

 Magiwji wa utangazaji nchini toka kulia Abdallah Idrissa Majura, Dunstan Tido Mhando, Salim Mbonde, Ahmed Kipozi na Charles Hilary  wakiwa nyumbani kwa marehemu aliyekuwa Mtangazaji maarufu wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo Tandika Maghorofani Dar es Salaam.
  
 Watangazaji, mafundi mitambo wacheza kandanda nyoya wa enzi hizo na viongozi wa soka wakipata picha ya kumbukumbu baada ya kujumuika na   ndugu, jamaa na marafiki  nyumbani kwa marehemu aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD), Ahmed Jongo  Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam.
Kwa Habari zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa Amani Mzee Ahmed Jongo.Michuzi Blog asante kwa picha nilikuwa sijawahi kuona picha wala kumuona Salim Mbonde!!TBC Taifa siku moja wawaalike hawa wakongwe watutangazie mechi moja walau dak kumi kumi walau,bado wanaweza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...