MUOGELEAJI nyota wa klabu ya kuogelea ya Morogoro, (Mis Piranha) , Dennis Mhini amepata nafasi ya kusoma na kujifunza mchezo wa kuogelea kwenye klabu maarufu ya St Felix ya Uingereza.

Dennis aliyeiwakilisha Tanzania katika michezo ya Olimpiki ya Vijana nchini, Argentina amepata nafasi hiyo baada ya kufikiwa viwango vilivyowekwa na shule hiyo chini ya kocha maarufu, Sue Purchese.Kigezo cha kwanza ni ubora wake katika mchezo kuogelea baada ya kufikia muda unaotakiwa na pili uwezo wake wa darasani.

Baba wa mchezaji huyo, Hamis Mhini alisema kuwa mwanaye pamoja na kutoweza kutwaa medali Argentina, alifanikiwa kupunguza muda wake wa kuogelea, jambo ambalo limewavutia sana walimu na kocha maarufu wa mchezo wa kuogelea nchini uingereza, Sue Purchase.

Mhini alisema kuwa hatua hiyo ni kubwa katika maendeleo ya mchezo wa kuogelea nchini kwani anaamini kuwa mwanaye ataiva na kuwa muogeleaji bora Tanzania na dunia.Alisema kuwa Dennis anapenda sana mchezo wa kuogelea na ndiyo maana waliamua kumpa nafasi ya kufanya kile ambacho anakipenda na kufikia kiwango cha kufuzu michezo ya Olimpiki ya Vijana iliyofanika mjini Buenos Aires.

Katika michezo hiyo, Dennis aliweza kushika nafasi ya tatu katika kundi la kwanza kweye staili ya freestyle ya mita 100 kwa kupata muda wa sekunde, 58.53 na pointi 514 na vile vile kumaliza katika nafasi ya tatu kwa upande staili ya backstroke kwa mita 50 kwa kutumia sekunde 29.79 na kupata pointi 525.Dennis alisema kuwa amefurahi sana kupata nafasi hiyo na kuahidi kufanya mambo makubwa kwa Taifa lake.

Alisema kuwa atahakikisha anakuwa na kiwango cha kufuzu katika mashindano mbalimbali duniani ikiwa pamoja na Mashindano ya Dunia, Jumuiya ya Madola na Olimpiki ya wakubwa.
Dennis Mhini (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na kocha Michael Livingstone (wa kwanza kulia) mara baada ya kuwasili kutoka Argentina. Wengine katika picha ni wanamichezo na viongozi.
Kocha wa mchezo wa riadha, Mwinga Mwanjala (kulia) akimkabidhi shada la maua, Dennis Mhini (wa tatu kushoto) mara baada ya kuwasili kutoka Argentina kwa ajili ya mashindano ya Olimpiki ya vijana. 
 Muogeleaji, Dennis Mhini (wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na wazazi wake, Hamis Mhini (wa kwanza kushoto), Bhoke Mukoji Mhini ( wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili kutoka Argentina kwa ya mashindano ya vijana ya Olimpiki. Wa nne kushoto ni kocha wa timu ya Taifa, Michael Livingstone ambaye anafuatiwa na Eugenia Kaitesi, Derick Mhini. Pia katika picha ni Deborah Mhini (katikati). 
Timu ya Tanzania iliyoshriki katika mashindano ya vijana ya Olimpiki katika picha ya pamoja na makocha wao na mkuu wa msafara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...