Na Takdir Ali-Maelezo Zanzibar
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kusini Abdul-aziz Hamad Ibrahim amewataka Viongozi wa Majimbo kusikiliza kero za Vijana ili kuweza  kuzipatia ufumbuzi.

Amesema vijana wanamchango mkubwa katika kuleta maendeleo hivyo iwapo Viongozi wanapita na kuwatatulia matatizo yanayowakabili wataweza kuongeza juhudi za kukipatia ushindi chama cha Mapinduzi ifikapo 2020.

Ameyasema hayo huko Tawi la CCM Kizimkazi Dimbani alipokuwa akizungumza na Vijana wa Tawi la Mpendae juu katika ziara ya kubadilishana mawazo na Vijana wa Tawi la CCM Kizimkazi Dimbani Wilaya ya Kusini.

Ameeleza kuwa Vijana wana matatizo mengi ikiwemo Ajira na elimu lakini baadhi ya Viongozi hawasaidii kitu chochote cha kuweza kujiendesha maisha  jambo ambalo linawavunja moyo na kuwarudisha nyuma kimaendeleo.

“Matatizo ya vijana ndani ya nchi  ni mengi ikiwemo ukosefu wa ajira hivyo viongozi wawasaidie vijana hao kwa kuwapa mitajiili waweze kujiendeleza katik maisha yao”. Alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha amewataka Vijana hao kuwaacha woga na kuwafikisha katika sehemu husika Viongozi watakaowabaini kwenda kinyume na Ilani ya Chama hicho.

Hata hivyo amewataka kujiendeleza kielimu ili wapate Ajira na kuisimamia Serikali mara baada ya Viongozi waliopo madarakani kumaliza muda wao wa Utumishi.

Amewapongeza Vijana wa Mpendae juu kwa kufanya ziara hiyo na kusema wamepata kukaa na kujadili njia za kuwaletea maendeleo na kukipatia ushindi cha Chama Cha Mapinduzi 2020.

Amefahamisha kuwa  Serikali inatumia gharama kubwa kutafuta Wataalamu nje ya nchi lakini iwapo Vijana watajiendeleza wataziba kuziba upungufu uliopo.

Mapema akitoa maelezo katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Tawi la CCM Mpendae Choum Fakih Muhudin amewapongeza Vijana wa Kizimkazi Dimbani kwa mapokezi mazuri na kuahidi kuendeleleza mashirikiano hayo yaliodumu kwa muda mrefu.

Amesema lengo la ziara hiyo ni kuweza kubadilishana mawazo juu ya njia mbalimbali za kuleta maendeleo kwa Vijana na kuzidi kukiletea ushindi chama cha Mapinduzi katika Chaguzi zote zinazoshiriki hapa nchini.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...