Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
MCHEZAJI wa kikosi cha Serengeti boys  Maurice Abraham ameanza majaribio katika klabu ya Midtjylland  nchini Denmark, ambao ndio mabingwa wa ligi kuu msimu uliopita 2017-18 nchini humo.

Ambapo Klabu hiyo ya Midtjylland ni matokeo ya  vilabu viwili mahasimu (Ikast na Herning) vilivyomua kuungana mwaka 1999 na kuunda klabu moja  iliyipanda daraja kucheza ligi kuu ya Denmark Danish Superliga  Mwaka 2000.

 Klabu hiyo  katika msimu wa 2014-15 ndio ilishinda taji la Danish Superliga kwa mara ya kwanza kabla ya kushinda tena taji  hilo mara ya pili msimu huo uliopita. 

Maurice a.k.a chuji ambaye ni Nahodha wa timu ya Taifa ya vijana U-17 alipata mualiko kutoka nchini Denmark kufanya majaribio katika klabu ya Midtjylland baada kuonyesha kiwango cha juu mno katika michuano ya kuwania Afcon 2019 kanda ya Cecafa ambapo Serengeti ilimaliza ikiwa imeshikilia nafasi ya tatu. 

Kocha mkuu wa Serengeti boys Oscar Mirambo ambaye pia ni kaimu mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, amesema kuwa  Chuji aliondoka Oktoba 7  ambapo alipata mualiko wa  kwenda nchini Denmark  kwa ajili ya majaribio. 

"Nyota wengi wa kikosi hicho cha vijana ambao ndio wenyeji wa fainali Za Afcon 2019 watakaondoka kwa utaratibu Kama uliofanywa kwa Maurice"amesema Mirambo. 

Kocha mirambo amesema "mialiko ipo mingi na baadhi ya wachezaji ila siwezi kusema nani anafuata sasa, lakini Maurice ameanza na tunasubiri taratibu  zikamilike kwa wengine ndipo tutaweka wazi"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...